Monday, June 15, 2020

Wapiga dili wajineemesha kupitia dhahabu ya DRC yasema ripoti

Wachimbaji wakiendelea kuisaka dhahabu. (Picha na Mtandao).
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Mashirika
Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebainisha kwamba, dhahabu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado inaendelea kusambazwa duniani kote, baada ya kusafirishwa kwa njia za magendo
kupitia nchi jirani za upande wa mpaka wake wa Mashariki.
Waziri wa madini wa Kongo, Willy Kitobo Samsoni alipoulizwa na shirika la habari la Reuters kuhusu ripoti hiyo amesema, hawezi kutoa takwimu kwa wakati huo juu ya usafirishaji wa madini kutoka Mashariki mwa nchi.
Wafanyabiashara ya magendo, walilieleza kundi la wataalamu kwamba mji mkuu wa Uganda wa Kampala ndiyo kitovu cha biashara ya dhahabu inayotokea Ituri.
Aidha, ripoti hiyo imeeleza kwamba, dhahabu inayosafirishwa kimagendo kutoka Kivu Kusini huwa inapelekwa nchi za Rwanda na Umoja wa Falme za Kiarabu.

No comments :

Post a Comment