Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba wakitilia saini
mikataba wa mradi wa mpango wa upelekaji wa huduma ya mawasiliano katika
maeneo yenye mawasiliano hafifu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba na Mtendaji Mkuu wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi.Justina Mashiba wakipongezana baada
ya kusaini mkataba wa wa mradi wa mpango wa upelekaji wa huduma ya
mawasiliano katika maeneo yenye mawasiliano hafifu.
******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Takribani wakazi laki 521,897
waishio vijijini wanatarajiwa kupelekewa huduma ya mwasiliano kupitia
mpango wa upelekaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo yenye
mawasiliano hafifu.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa hafla
ya utiaji saini mkataba wa mradi huo kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa
wote (UCSAF) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) iliyofanyika
katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es
Salaam.
Amesema mradi huo utanufaisha kata
32 zenye vijiji 45 katika maeneo ya mipakani na Kanda Maalumu kwa
gharama za shilingi Bilioni 5.1, ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya tano
ya mradi huo.
“Ninashauku kubwa kuona huduma
zote wanazofurahia watu wa mijini ikiwemo kupiga na kupokea simu,kutuma
na kupokea fedha na matumizi ya mtandao wa intaneti zinawafikia pia watu
wa vijijini kabla ya kumalizika mwaka 2021”. Amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesema kuwa Serikali kupitia
UCSAF imefanikiwa kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi wengi
awali hawakuwa na huduma hiyo muhimu.
Aidha Mhandisi Kamwelwe ameitaka
NEMC kuharakisha mchakato wa kupatikana kibari cha mazingira ili mradi
huo uweze kutekelezwa kwa haraka.
No comments :
Post a Comment