Mkurugenzi wa Chama cha waandishi
wa habari wanawake Tamwa-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa mara baada ya kuwasili
katika moja ya shamba linalomikiwa na wajasiriamali wanawake huko
Bumbwini Mkoa wa kaskazini Unguja ambapo shamba hilo limepangwa kutumika
kwa kilimo cha mboga mboga.
Baadhi ya wanakikundi kutoka
shehia ya Bumbwini Mafufuni Unguja wakiendelea na shughuli zao za
uzalishaji wa sabuni ya maji ambapo sabuni hizo zimekua na soko kubwa
hisi sasa kufuatua kutumika kama kinga dhidi ya maradhi ya korona.
…………………………………………………………………..
Na Masanja Mabula , Zanzibar,
MKURUGENZI wa Chama cha waandisi
wa habari wanawake Tamwa—Zanzibar Dr Mzuri Issa amewataka wajasiriamli
kisiwani Unguja kutokata tamaa licha ya uwepo wa
changamoto mbali
mbali katika harakati zao za kila za uzalishaji wa bidhaa.
Dkt,Mzuri aliyasema hayo jana
wakati wa ziara maalumu ya kutembelea vikundi katika shehia mbali mbali
za mkoa wa kaskazini kwa lengo la kujionea ni kwanamna gani
wajasiriamali hao wanafanyia kazi elimu wanayopewa kupitia chama hicho.
Aliwataka wajasiriamali hao
kutokata tamaa licha ya changamoto za hapa na pale badala yake
wajitahidi zaidi wakiamini kuwa umoja wao ndio suluhisho la changamoto
hizo.
Alisema kuna jitihada kubwa
zimefanywa na wajasiriamali na wanapaswa kuungwa mkono kwa kuwa lengo
lao ni moja kujikwamua na umasikini.
Aidha alisema Tamwa-Zanzibar
itaendelea kufanya kila jitihada zenye lengo la kuhakiksha wanawasaidia
wajasiriamali hao ili waweze kutimiza ndoto zao.
Katika hatua nyengine aliwataka
wanawake kuzitumia fursa mbali mbali kwenye jamii ikiwemo za kushiriki
mara pale muda utakapofika katika kugombe anafasi mbali mbali za kisiasa
kupitia maeneo yao.
Aliwataka wanawake hao kuacha
kubweteka na kudhani nafasi za uongozi ni za wanaume pekee badala yake
wanapaswa kujitambua na kuwa tayari muda wowote.
Awali afisa uwezeshaji wanawake
kiuchumi Tamwa-Zanzibar Nairat Abdalla aliwataka akinamama hao
kuridhika na masoko ya bidhaa zao katika maeneo husika badalka yake
wanapaswa kufikiri mbali zaidi.
Alisema kuna fursa nyingi za masoko kupitia bidhaa hizo hivyo ni vyema kuyatumia mask ohayo ali waweze kujingizia kipato zaidi.
Kwa nyakati
tofauti baadhi ya wajasiriamali hao walisema wamekua wakikumbana na
ugumu katika utendaji wao wa kazi hususani za kilimo kutokana na maeneo
mengi kukosa maji ambayo yangewafanya waweze kulima kwa urahisi katika
kilimo cha mboga mboga.
No comments :
Post a Comment