Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa
ya Mkoa ya Amana Dr. Amani Malima, aliyevaa shati akipokea gallon
ya lita 5 za vitakasa mikono (sanitizer) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa
TMRC Oscar Mgaya wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano ya mchango huo wa
Vitakasa mikono
……………………………………….
TMRC imetoa msaada huo kwa
hospitali ya Serikali ya Amana. Msaada huo ni gallons 50 za lita 5 za
vitakasa mikono (sanitizer) ambazo kwa ujumla wake ni lita 250.
Msaada huo ulipokelewa na Mganga
Mkuu wa hospitali hiyo ya Amana Dr. Amani Malima, ambaye wakati wa
kupokea msaada huo ameishukuru serikali kwa ushirikano wanaopata
kutokana na hospitali hiyo kuteuliwa kuhudumia wangonjwa wa CORONA, Pia
Dr. Amani ameishukuru Taasisi ya mikopo ya nyumba Tanzania (TMRC) kwa
mchango walioutoa wa lita 250 za vitakasa mikono (sanitizer) amesema
mchango huo utawasaidia sana hasa watoa huduma wa hospitalini katika
kujilinda na maambukizi ya CORONA, pia ametoa wito kwa taasisi zingine
kuiga mfano uliotolewa na TMRC katika kuhakikisha tunalimaliza janga
hili la ungonjwa wa Corona, amesema mpaka sasa wamebakiwa na mgonjwa
mmoja tu mwenye maambukizi ya virusi vya CORONA Pia ametoa wito kwa
jamii kuendelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi ya
ugonjwa wa corona na kuhakikisha janga hili tunalimaliza kabisa.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji
Mkuu wa TMRC Oscar Mgaya alisema kuwa msaada huu ni mchango wa taasisi
hiyo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona. Ndugu Mgaya aliisifu
sana hospitali ya Amana kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi
ya ugonjwa huo. “Sisi kama taasisi tuliona ni muhimu tutoe mchango huu
mdogo kwa hospitali ya Amana kama namna ya kuwasaidia na mapambano dhidi
ya ugonjwa huo”
No comments :
Post a Comment