Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Dkt. Avelina Mgasa.
……………………………………………………………………………………………………
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama
ulio chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto umetoa rai kwa Wananchi kutoa taarifa kwa wanaouza damu ili
wachukuliwe hatua kali za kisheria kwani damu inatolewa bure kwa
wahitaji.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni
na Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama,
Dk. Avelina Mgasa wakati wa Semina iliyofanyika kwa njia ya mtandao na
kushirikisha Waandishi wa habari za Afya zaidi ya 30 kutoka maeneo
mbalimbali ya Tanzania ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya
Wachangiaji damu Duniani hapo Juni 14.
Dkt.Mgasa alisisitiza juu ya
Wananchi kuripoti endapo watakutana na vitendo hivyo vya kuombwa pesa
ili kupatiwa damu kwani tayari sheria zimeanza kuchukuliwa kwa watendaji
wasio waaminifu.
“Wananchi wasiogope kusema. Tanzania bado hatujaanza kuuza damu.
Damu ni bure kama watakutana na vitendo vya kuombwa pesa basi waripoti kwa Mganga mkuu wa kituo, Hospitali husika.
Kwa sasa tunao mfano mzuri kwa hatua zilizochukuliwa ikiwemo kule Wilaya ya Kongwa”. Alisema Dkt. Mgasa.
Kwa sasa tunao mfano mzuri kwa hatua zilizochukuliwa ikiwemo kule Wilaya ya Kongwa”. Alisema Dkt. Mgasa.
Aidha, Dkt. Mgasa alitoa wito kwa watoa huduma kwa Mgonjwa anapohitaji damu na kama ipo apewe.
“Hatuwezi kuacha mtu apoteze maisha kwa kukosa damu.
Ndio maama tunahamasisha watu kuchangia damu kwa hiyari ili kuokoa ndugu ama jamaa zetu watakapata tatizo” alisema Dk. Mgasa.
Ndio maama tunahamasisha watu kuchangia damu kwa hiyari ili kuokoa ndugu ama jamaa zetu watakapata tatizo” alisema Dk. Mgasa.
Aidha, akiwasilisha mada kwa kina namna ya Mpango wa Taifa wa damu salama;
Alisema kuwa kutokana na janga la
mlipuko wa virusi vya corona (COVID-19) nchini, kiwango cha uchangiaji
damu kimeshuka kutoka chupa 31,502 za mwezi Februari, chupa 25,737 za
mwezi Machi hadi kufikia chupa 22,044 Mwezi Aprili.
“Hali hiyo imechangiwa na shule na vyuo kufungwa hivyo kukosa fursa za kukusanya damu katika ofisi mbalimbali.
“Kingine ambacho kimesababisha
ukasanyaji wa damu kuwa mdogo ni zuio la mikusanyiko kutokana na
maelekezo ya Serikali katika kupambana na Covid-19 kwani maeneo hayo
ndiyo yamekuwa yakitegemewa zaidi”. Alisema Dk. Mgasa.
Dk Mgasa amesema kwa sasa wamejipanga katika kuhakikisha watu
wanachangia damu katika mazingira salama ambayo yatawawezesha kujikinga
na Covid-19.
“Kutokana na hilo basi uhitaji wa
damu ni mkubwa sisi kama damu salama tumejipanga kwani uchangia wa damu
ni tendo salama na mpango umeweka mikakati mbalimbali ya kuzuia
maambukizi ya Virusi vya Corona katika vituo vya kuchangia damu.
“Tumuweka maji tiririka na sabuni
kwaajili ya kunawa mikono, Vitakasa mikono, Vifaa kinga kwa watumishi
kama barakoa, apron/koti, gloves, na goggles, Thermo scanner kwa ajili
ya kupima jotoridi la mwili kwa kila mchangia damu.
“Tunatakasa vitanda na vifaa
vinavyotumika na wachangia damu, mpangilio unaozingatia umbali kati ya
mtu na mtu (social distance)”. Alieleza Dk Mgasa.
Katika maadhimisho ya mwaka huu Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu anatarajiwa kuongea na Wananchi na kuwashukuru wachangia damu.
Dk. Mgasa alisema kampeni kwa
mwaka huu yenye Kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni “Damu Salama
Inaokoa Maisha”- (“Safe Blood Saves Lives”) ikiwa na malengo ya
kukusanya chupa za damu 24,800.
Dk. Mgasa alimalizia kwa kutoa
wito kwa wachangia damu kukitokeza kwa wingi kuchangia kwa hiyari kwenye
maeneo yote ya Kanda hapa Nchini huku kwa Kanda ya Mashariki ikiwemo
Dar es salaam yenye vituo 10 ndio yenye uhitaji mkubwa zaidi.
“Mahitaji ya damu ni makubwa zaidi kanda ya Mashariki.
Chupa nyingi za damu zinahitajika na zinatumika kwa wingi ikiwemo Hospitali ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, taasisi ya Mifupa (MOI) na maeneo kwingine”. Alisema.
Chupa nyingi za damu zinahitajika na zinatumika kwa wingi ikiwemo Hospitali ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, taasisi ya Mifupa (MOI) na maeneo kwingine”. Alisema.
Alivitaja vituo hivyo vya kuchangia damu ni pamoja na:
Ofisi zote za Kanda za mpango wa Taifa wa Damu Salama, Hospitali zote za Rufaa za Mkoa, Hospitali za zote Halmashauri nchini.
Ofisi zote za Kanda za mpango wa Taifa wa Damu Salama, Hospitali zote za Rufaa za Mkoa, Hospitali za zote Halmashauri nchini.
“Kwa Dar es Salaam tuna vituo 10 ambavyo ni Hospitali za Rufaa za Mkoa Amana,Mwananyamala na Temeke.
Zipo pia Hospitali ya Jeshi
Lugalo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Mbweni, Vijibweni na
Mbagala Rangi Tatu” alisema Dkt. Mgasa.
Akimalizia katika mafunzo hayo,
alibainisha kuwa zoezo la utoaji damu ni umakini na hivyo amewatoa hofu
wananchi hasa kipindi ambacho dunia inaendelea kuoambana na COVID-19.
“Kabla ya kuchukua damu unadodoso utapitia. Na tutakushauri.
Suala la mtu aliyeumwa Corona anaweza kuchangia damu endapo atathibitishwa amepona.
Kw sasa haijathibitika kitaalam kama Corona inaambukizwa kwa njia ya damu.
Kw sasa haijathibitika kitaalam kama Corona inaambukizwa kwa njia ya damu.
Mpango wa taifa qa damu salama
tunashauri aliyeumwa mfano Typhoid anatakiwa achangie damu baada ya
kupita miezi sita (6) lakini pia kwa mwaanamke aliyeingia Headhi
anapoteza damu nyingi inapendeza achangie kila miezi minne” alisema Dkt.
Mgasa.
Aidha, aliwashukuru Wananchi kuendelea kujitolea damu ambapo zimekuwa msaada mkubwa wa kuokoa maisha ya watu.
No comments :
Post a Comment