Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.Mohamed Janabi akizungumza na waajiriwa wapya saba walioajiriwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa wapya saba walioajiriwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kupangiwa kazi katika
Taasisi hiyo mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu kwa waajiriwa hao leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa JKCI Agnes Kuhenga.
Picha na JKCI
***************************
Na Mwandishi Maalum – Dar es Salaam
03/06/2020
WAAJIRIWA wapya katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),
wametakiwa kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii ili kuendeleza juhudi za
kuokoa maisha ya watu wanaokabiliwa na magonjwa ya moyo wanaofika
kupata matibabu katika taasisi hiyo.
Rai
hiyo imetolewa mapema leo na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa
Mohamed Janabi alipokuwa akizungumza na waajiriwa wapya saba
walioajiriwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo.
“Taasisi
hii imepata mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa hadi sasa, baadhi
yenu mmekuwa sehemu ya juhudi hizi, kwa sababu kwa nyakati mbalimbali
mmewahi kujitolea kufanya mafunzo kwa vitendo hapa”.
“Kwa
juhudi zile zile endeleeni kuchapa kazi, kila mmoja awajibike katika
nafasi yake, mtaona faida ya kazi na juhudi zenu, hakikisheni mnawahi
kazini, binafsi huwa sitaki kusikia habari za foleni, mvua kwamba ni
sehemu ya sababu ya kuchelewa kufika kazini,” amesisitiza.
Ameongeza
“Tuna mafanikio makubwa, tangu kuanzishwa kwa Taasisi hii, miaka minne
ya utendaji kazi wetu vifo vilivyotokea katika chumba cha upasuaji mdogo
wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo kwenye paja ni asilimia 1.5
yaani sawa na wagonjwa wanane tu waliopoteza maisha katika kipindi chote
hicho.
“Tumeweza
kupandikiza vifaa visaidizi vinavyousaidia moyo kufanya kazi
vizuri (Pacemaker) kwa wagonjwa 56, CRTD kwa wagonjwa wagonjwa 11,
tumevuna na kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Graft – CABG) wagonjwa
82 na tumezibua valvu zilizokuwa zimeziba bila kufanya upasuaji wa
kufungua kifua kwa zaidi ya wagonjwa 1,000 hadi sasa,” amebainisha.
Amewataka
waajiriwa hao kutosita kuuliza wale waliowatangulia kazini mahala
popote watakapokutana na changamoto mbalimbali ili kuweza kuzitatua na
kuzingatia uvaaji nadhifu wa mavazi yenye staha.
Akizungumza
kwa niaba ya waajiriwa wapya wenzake, Daktari Winnie Masakuya amesema
wapo tayari kufanya kazi kwa juhudi na maarifa waliyojaliwa na Mwenyezi
Mungu katika kuwahudumia wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
“Hatutaiangusha
Taasisi yetu,” amemhakikishia Prof, Janabi katika kikao hicho ambacho
pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha wa JKCI,
Agnes Kuhenga.
No comments :
Post a Comment