Serikali
imezindua rasmi mwongozo wa uendeshaji wa Shughuli za Utalii nchini
Tanzania wakati huu wa janga la Corona na kuwataka wadau sekta hiyo
kuzingatia
matakwa yaliyo katika mwongozo huo ili kulinda usalama wa Watanzania na watalii wanaowasili nchini kutembelea vivutio vilivyopo.
matakwa yaliyo katika mwongozo huo ili kulinda usalama wa Watanzania na watalii wanaowasili nchini kutembelea vivutio vilivyopo.
Akizindua
mwongozo huo jana jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla amewataka wadau wote wa Sekta watimize wajibu wao kwa
kuhakikisha wageni wote wanaoingia nchini wanakuwa salama na wanaondoka
salama pasipo kuambukizwa au kuambukiza wengine virusi vya Corona.
Dkt.
Kigwangalla amesema Serikali imeamua kuzindua rasmi mwongozo huo ili
kuilinda Sekta ya Utalii pamoja na afya za wadau wote wanaohusika na
sekta hiyo na kuongeza kuwa hatua hiyo itaongeza na kujenga imani ya
wageni wanaoitembelea Tanzania kutokana na masharti ya kiafya
yaliyoainishwa katika mwongozo huo ambayo watoa huduma za utalii
wanatakiwa kuyazingatia.
Ameongeza
kuwa mwongozo huo huo utaisaidia biashara ya Utalii kuanza upya wakati
huu wa janga la CORONA ambapo Tanzania imeamua kufuangua mipaka yake
kufuatia baadhi ya nchi zikiwemo za Ulaya kuanza kufungua anga kwa
kuruhusu mashirika makubwa ya ndege kuanzisha safari za ndege za abiria
kutua katika nchi hizo kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Amebainisha
kuwa Tanzania imeondoa masharti mengi ambayo yalikuwa yakikwamisha
watalii wengi kuja nchini Tanzania likiwemo lile la mtalii kukaa
Karantini kwa muda wa siku 14.
Dkt.
Kigwangalla amewahakikishia wageni mbalimbali wanaopanga safari zao
kuja nchini Tanzania waje bila hofu yoyote kwa kuwa Tanzania ni nchi
salama.
MWISHO.
No comments :
Post a Comment