Naibu
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Ilemela
Dkt.Angeline Mabula akizungumza na wananchi waliohudhuria katika zoezi
la ugawaji hati kwa halmashauri ya Ilemela lililofanyika halmashauri
hapo. Picha na Judith Ferdinand.Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza wamepatiwa Hati Miliki za Ardhi huku halmashauri zote nchini zikitakiwa kuacha kufanya kazi na makampuni ya upima ambayo hayana uwezo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Ilemela
Dkt.Angeline Mabula akizungumza na wananchi waliohudhuria katika zoezi
la ugawaji hati kwa Halmashauri ya Ilemela lililofanyika halmashauri
hapo. Picha na Judith Ferdinand.
Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi jijini Mwanza iliyoambatana na
ugawaji wa hati miliki kwa wananchi wa halmashauri hizo mbili, Naibu
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina
Mabula amesema halmashauri zinapaswa kuchunguza na kupitia upya mikataba
ya makampuni ya upimaji ambayo hayana uwezo na kuacha kufanya nazo kazi
kwani hali hiyo zinasababisha usumbufu kwa wakazi wanotaka kupimiwa
maeneo yao.
,Baadhi
ya wananchi waliohudhuria katika zoezi la ugawaji hati kwa halmashauri
ya Ilemela lililofanyika halmashauri hapo. Picha na Judith Ferdinand.
“Nitoe rai kwa halmashauri zote nchini, tusiingie mikataba na
makapuni ambayo hayana uwezo, tunahitaji makampuni yenye uwezo ambayo
yanaweza kuendelea kupima huku wananchi wakilipia ila yale ambayo mpaka
mwanachi alipie kwanza ndio ardhi ipimwe hayafai, Halmashauri
zimeshapewa maelekezo sasa hivi kazi inayofanyika ni kupitia mikataba
yao upya na kuivunja,” amesema Dkt.Angeline.
Naibu
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Ilemela
Dkt.Angeline Mabula akizungumza na wananchi waliohudhuria katika zoezi
la ugawaji hati kwa halmashauri ya Ilemela lililofanyika halmashauri
hapo. Picha na Judith Ferdinand.
Akimweleza Naibu Waziri, Kyando amesema “Ulitupa maelekezo ya kuandaa
hati kwa ajili ya walimu na wafanyakazi ambao wapo tayari kuchangia
fedha kwa ajili ya upimaji na hati tumeisha andaa viwanja 525 na walimu
zaidi ya 400 wameisha vilipia.”Ofisa Mipango Miji wa Jiji la Mwanza, Hosiana Kusiga amesema lengo lilikuwa ni kukusanya bilioni 6 katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 lakini hadi sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 3 sawa na asilimia 52.9.
Baadhi ya wananchi wa Ilemela na Nyamagana waliopatiwa hati, wamewashauri wananchi wenzao kufuata taratibu na sheria zilizowekwa kwa kuhakikisha wanapimiwa na kumilikishwa viwanja vyao kisha wapatiwe hati ambayo ndio kitu wanachoweza kuringia na kuishi bila hofu wala wasiwasi na kumiliki kwa uhuru ardhi waliojaliwa na Mungu.
No comments :
Post a Comment