Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
RAIS Dk.John Magufuli amesema kwamba Corona imepungua kwa kiasi kikubwa nchini na hivyo shule za chekechekea na shule za msingi siku za hivi karibuni.
Ametoa kauli hiyo leo Juni 5 Mjini Dodoma wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) uliofanyika Uwanja wa Jamhuri na kuhudhuria na viongozi wa ngazi mbalimbali Serikalini pamoja na walimu wa kada zote.
Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa anamshukuru Mungu na anawashukuru walimu wote nchini kwa kazi kubwa wanayofanya.Pia kwa namna wanavyounga mkono katika masuala mbalimbali huku akiwaambia kuongoza ni changamoto kubwa, walimu ni mashahidi katika vita ya kiuchumi ina mambo mengi.
"Tunamshukuru Mungu na nawashukuru sana walimu tumeshinda vita dhidi ya Corona, tukaendelee kushinda na mimi nina uhahika siku za hivi karibuni kwa jinsi mambo yanavyokwenda baaada ya kufungua vyuo , tutafungua shule zote kuanzia chekea na shule za msingi.Tuko mbioni tutafungua shule zote kwasababu walimu wa Tanzania wanapenda kazi,"amesema Rais Magufuli.
Awali akifafanua zaidi kabla ya kuelezea hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kufungua shule zote, Rais Magufuli amesema "Labda nikumbushe kidogo juhudi ambazo tunafanya Serikali katika kujitegemea na kuleta maendeleo kupitia miradi mbalimbali ambayo mnaiyona katika maeneo yenu mnayotoka.
"Ni kwasababu tumeimarisha ukusanyaji wa mapato.Tulipoingia mdarakani makusanyo kwa mwezi yalikuwa shilingi bilioni 800 kwa sasa hivi na kwenye miezi miwili iliyopita makosanyo kwa mwezi yalifikia mpaka trilioni 1.9, kwa nchi yoyote inayojitegemea inatengeneza maadui na ndio maaa mtaona wakati tunaingia madakarani tuliambiwa Tanzania tuna zika, tuna ugonjwa unaoitwa Zika.
"Aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamtimua , na bahati mbaya ni Mgogo, baada ya kumfukuza kazi siku chache akateuliwa na wale waliokuwa wamemtuma atangaze kuna Zika siku chache wakamteua kuwa Mkurugenzi , kuanzia tulipomtoa karibia miaka mitano hatutawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania,"amesema.
Rais Magufuli amesema baade tukaambiwa kuna Ebola wakati hakuna Ebola wala hawara yake Ebola lakini waling'ang'ana lakini waliwaambia hakuna Ebola na kweli hakukua na Ebola. "Hatujaona mgonjwa wala nani amekufa kwa Ebola hapa Tanzania.
"Hilo nalo likapita , umekuja ugonjwa wa Corona ,walikuwa wanazungumza na ninyi mmesikia kuwa maiti zitazagaa kwenye barabarani hasa Afrika wao walikuwa watabiri walishindwa kuelewa kuwa Mungu wetu analipenda Taifa hili la Tanzania.
"Tuliomba siku tatu Corona imekwisha. Nilikuwa napata taarifa za Waziri wa Afya juzi anasema Dar es Salaam kulikuwa na wagonjwa wanne lakini uzushi utatolewa wa kila aina, ndugu zangu ninyi walimu yale yanayoitwa yanayovaliwa mdomoni , mabarokoa au, hakuna hata aliyevaa leo tunaonana tu hapa kawaida.
No comments :
Post a Comment