Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa
cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa Masinki ya kunawia mikono bila kugusa koki ambayo ni sehemu
ya kifaa cha kisasa cha kunawia mikono kilichotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
inayotengeneza vinywaji vya Diamond Rock na Hansons Choice kwa ajili
ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 4,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (katikati) akikata utepe wakati
akipokea kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa
vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona kutoka Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga, Gasper Kileo akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab
Telack (aliyevaa kilemba cha bluu) namna ya kunawa mikono kwa kutumia
kifaa cha kisasa cha kunawia mikono.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha
kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha
kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akinawa mikono kwa kifaa cha
kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akinawa mikono kwa kifaa
cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni
ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
kwa mchango wa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu palipowekwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono
iliyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African
Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.

Muonekano wa sehemu wa tanki la maji ambalo ni sehemu ya kifaa cha
kisasa cha kunawia mikono kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji
Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu palipowekwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono
iliyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African
Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa kwa ajili ya kujikinga na COVID-19 ikiwemo
Vitakasa mikono,barakoa,gloves, pamba,cord clamp na pulse Oximeter
vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2 vilivyotolewa na Kampuni ya
Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga
katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga, Gasper Kileo akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Zainab Telack (aliyevaa kilemba cha bluu kushoto) kifaa cha
kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa vya kujikinga na
Maambukizi ya Virusi vya Corona katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga, Gasper Kileo akiipongeza serikali inayoongozwa na Rais Dkt.
John Pombe Magufuli namna ilivyopambana na ugonjwa wa COVID – 19.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (wa tatu kulia) akiishukuru
Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa mchango wa
vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T)
Limited Shinyanga, Gasper Kileo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Zainab Telack sabuni ya kunawia mikono ili kukabiliana na COVID - 19
katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T)
Limited Shinyanga, Gasper Kileo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Zainab Telack Vitakasa mikono ili kukabiliana na COVID - 19 katika
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Timoth Sosoma akiishukuru
Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa msaada wa
vifaa vya kujikinga na COVID- 19 ambavyo vitasaidia katika kukabiliana
na ugonjwa wa Corona katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni
ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga inayotengeneza vinywaji vya Diamond Rock na
Hansons Choice imekabidhi msaada wa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona vyenye thamani vya shilingi Milioni 8 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Vifaa
vilivyotolewa na Kampuni hiyo ya East African Spirits (T) Limited
Shinyanga ni pamoja na kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa
koki chenye thamani ya shilingi Milioni 6.8 kikiwa na masinki matano na
tenki la maji lenye ujazo wa lita 1000 na vifaa vingine vya kujikinga na
COVID-19 ikiwemo Vitakasa mikono,barakoa,gloves, pamba, sabuni za
maji, cord clamp na pulse Oximeter vyenye thamani ya shilingi milioni
1.2.
Msaada huo umekabidhiwa leo Alhamis Juni 4,2020 na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo
kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Akikabidhi vifaa hivyo, Gasper Kileo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (MNEC) amesema vifaa hivyo vitatumika katika
kuiongezea nguvu serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
“Ninaishukuru sana serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Amiri
Jeshi wetu Mkuu, Rais wetu Mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli namna
ilivyopambana na ugonjwa wa COVID – 19. Tumepambana na COVID-19 tofauti
na nchi zote duniani na sasa wote ni mashahidi kwenye vyombo mbalimbali
vya habari na Mitandao ya Kijamii kwamba dunia sasa inaangalia Tanzania
imefanya nini kuiondoa Corona. wenzetu ndiyo wanafuta kile tunachofanya
Tanzania”,amesema Kileo.
“Nimpongeze pia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Zainab Telack kwa namna mnavyopambana dhidi ya Corona. Lakini
pia niwapongeze Madaktari wetu wote nchi nzima mmepambana kwa
kushirikiana na serikali na Mungu ametusaidia tumeweza. Naomba tuendelee
kupambana mpaka pale Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli
atakaposema silaha zetu tuziweke chini”,ameongeza Kileo.
Mkurugenzi huyo pia amewashauri wananchi kuendelea kunawa mikono na
kwamba zoezi hilo liwe endelevu hata siku watakapotangaziwa kuwa Corona
imefutika nchini Tanzania.
Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
ameishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa
mchango huo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali
katika mapambano dhidi ya Corona.
“Mheshimiwa MNEC uliniambia utaleta vifaa kwa ajili ya kupambana na
Corona lakini sikujua kama utaleta vikubwa namna hii. Umetuwekea masinki
ya kunawia mikono na tenki kubwa la maji na umeweka hadi kivuli ili
watu wetu wanaponawa mikono wawe kivulini. Mwenyezi Mungu akubariki sana
na abariki Biashara yako na shughuli unazofanya ziendelee na kukua ili
uweze kutupa misaada mingine zaidi”,amesema Telack.
“Kimsingi mimi nimepokea vifaa hivi kwa niaba ya wananchi lakini hawa
wananchi wanaonawa hapa wataendelea kukuombea kwa Mungu. Umetengeneza
kitu kikubwa sana na pengine ndiyo maana walikuchagua kuwa MNEC wao hata
wale wasiokuwa wa CCM sasa wanaona jinsi viongozi wa CCM na serikali ya
CCM inavyojali wananchi. Huu ni mfano wa kutosha,niombe na viongozi
wengine waige mfano wako”,amesema Mkuu huyo wa mkoa.
“Umeenda kisasa zaidi,umetuletea vifaa vya kisasa,na naomba uongozi
wa hospitali hii uweke mtu wa kuwaelekeza wananchi namna ya kutumia
kifaa hiki, wasianze kugusa gusa wakavunja hapa,wajue kwamba akisogeza
mikono yake maji yanatoka. Na pengine hapa patakuwa mahali pa kujifunzia
masuala ya teknolojia ya kisasa.
Yaani MNEC unafundisha watu teknolojia ambazo zipo,wataambiana
ukienda hospitali,ukisogeza tu mkono maji yanatoka,yaani hiyo nayo ni
sehemu ya kujifunzia. Ninategemea tutapata wageni wengi zaidi,wengine
watakuja kunawa tu mikono ili waone jinsi maji yanavyoka bila
kugusa,wananchi watakuja kujifunza. RMO naomba vifaa hivi vitunzwe ili
visiharibike”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuendelea
kunawa mikono mara kwa mara ili kupunguza maradhi mengine yanayotokana
na kutozingatia taratibu za afya
“Kunawa mikono ni ustaarabu. Sasa hivi siyo COVID -19 peke yake
tumegundua kwamba kunawa mikono kunatupunguzia maradhi mengine kama vile
tumbo na kuharisha,huko wodini sasa hivi watu waliokuwa wanakuja kwa
matatizo ya tumbo na kuhara wamepungua kwa kiasi kikubwa sana”,amesema.
“Niwaombe wananchi wa Shinyanga hii tabia ya kunawa mikono iwe
endelevu siyo kwa sababu ya Corona tu,hata baada ya Corona unaingia
hospitali nawa mikono yako,unaingia sokoni nawa mikono yako ili pia
tuweze kupunguza maradhi mengine yanayotokana na kutozingatia taratibu
za afya”,ameongeza Telack.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Timoth Sosoma
ameishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa
msaada huo na kueleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia katika kukabiliana na
ugonjwa wa Corona huku akiwataka wananchi wasiwe wagumu kunawa mikono.
No comments :
Post a Comment