Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na uongozi
wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kabla ya kikao cha Mene4jimenti ya
Mfuko huo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akimzikiliza Mkurugenzi
wa NHIF Bw. Bernald Konga kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo
wakati akizungumza na uongozi huo..
Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernald
Konga akiandika baadhi ya mambo wakati Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Wanawake,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu alipozungumza nao.
…………………………………………………………………………………….
Na.WAMJW,DSM
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) imetakiwa kutatua malalamiko ya upatikanaji wa
baadhi ya dawa na
vipimo kwa wananchi wenye bima ya afya.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa
kikao na Menejimenti ya Mfuko huo katika ofisi ndogo za wizara zilizopo
jijini, Dar es Salaam.
“Kumekuwepo na malalamiko ya
upatikanaji wa baadhi ya dawa na vipimo kwa watu wenye kadi za bima pia
ucheleweshaji wa malipo ya watoa huduma za afya” Alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameutaka mfuko
huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na
mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa katika vifurushi vya bima ya
afya.
“Tatueni malalamiko yote kwa wakati ili wananchi wafurahie vifurushi vyote watakavyojiunga navyo”.Alisisitiza Waziri Ummy
Kikao hicho pia kiliangalia
mwenendo wa utoaji wa huduma za bima za afya zinazotolewa na mfuko huo
ambapo kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Benard Konga,
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, na
Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
No comments :
Post a Comment