………………………………………………………………….
Naibu Waziri Kilimo Mhe.Hussein
Bashe leo amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Mpango wa Chakula
Duniani (WFP) Bw.Michael Dunford Ofsini kwake ambapo walifanya
mazungumzo mafupi.
Wakiwa katika kikao hicho kifupi
Bw.Michael amesema ujio wake umelenga kuagana na uongozi wa wizara kwa
niaba ya wafanyakazi wote kwa kuwa amepangiwa kazi nyingine ya kuwa
Mwakilishi wa WFP katika nchi za Afrika mashariki ambapo makao makuu
yake yapo jijini Nairobi Nchini Kenya.
Bw. michael ameleza kufurahishwa
na utendaji kazi wa serikali kupitia wizara ya kilimo ambapo miradi
mingi chini ya WFP ilitekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Pia amemshukuru Mhe.Bashe kwa
namna wizara walivyoweza kushirikiana naye wakati wa uongizi wake ambapo
amekiri kwamba ushirikiano huo ulisababisha kutekeleza majukimu yake
kwa ufanisi zaidi alisema Bw.Michael.
Naye Naibu Waziri Kilimo Mhe.
Bashe mara baada ya shukrani hizo amemuomba Bw. michael kufikisha ujumbe
Wfp kwamba waongeze wigo wa ununuzi wa mazao ya kilimo nchini hapa
yakiwemo mtama na ngano badala ya mahindi peke yake ili wakulima waweze
kupata fursa nyingine ya soko la mazao hayo.
“Tumekuwa tukifanya biashra na WFP hasa ya mazao ya mahindi kwa muda sasa kupitia wakala wa uhifadhi wa Chakula nchini NFRA jambo ambalo limesaidia kuongeza soko na ubora wa mahindi kwa wakulima lakini tunadhani sasa muongeze wigo katika kununua mazao mengine kama ngano na mtama kwakuwa mahitaji yake ni makubwa,, alisema Mhe. Bashe.

Aidha Mhe.Bashe alimalizia kwa
kusema kwamba Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Shirika hili
kwa kuwa wamekuwa wadau wakubwa katika kushughulikia masuala muhimu ya
usalama wa Chakula na lishe katika taifa letu.
No comments :
Post a Comment