NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto)
akiongoza kikao baina ya Menejimenti ya NSSF na uongozi wa Knight
Support.
Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa
NSSF, Bw. Suleiman Msangi (aliyesimama), akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira
Mhe. Anthony Mavunde, taarifa ya kuchelewa kuleta michango kwa Kampuni ya Night Support.
Mhe. Anthony Mavunde, taarifa ya kuchelewa kuleta michango kwa Kampuni ya Night Support.
Mhasibu wa Kampuni ya Ulinzi ya
Knight Support (mwenye shati nyeupe aliyekaa) pamoja na Mkurugenzi wa
Kampuni hiyo Bresing Kachambwa (aliyekaa kushoto) wakiwa chini ya Ulinzi
wa Polisi, kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa Kituo cha Polisi
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi wa
Knight Support (wa kwanza kulia), Bresing Kachambwa na Wahasibu wa
kampuni hiyo wakiwa kwenye gari ya Polisi, Makao Makuu ya NSSF baada ya
kukamatwa kutokana na kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wa
kampuni hiyo inayofikia Tzs. bilioni 8.417.
………………………………………………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Serikali
imeelekeza orodha ya wadaiwa sugu na waajiri wote wasiowasilisha
michango ya
wafanyakazi wao kuchukuliwa hatua za kisheria na wahusika
kufikishwa mahakamani mara moja.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na
Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati wa kikao baina ya Menejimenti ya NSSF,
Kampuni ya Knight Support na Wafanyakazi wa Knight Support juu ya
mustakabali wa malimbikizo ya wasilisho la michango ya wafanyakazi
pamoja na tozo ya adhabu inayofikia takribani Tsh 8.4Bn ikiwa ni
michango ya kuanzia mwaka 2011-2018.
Akizungumza
Mhe.Mavunde ametoa rai kwa waajiri wote nchini ambao hawawasilishi
michango ya wafanyakazi wao kujisalimisha mapema NSSF kabla ya
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mhe. Mavunde
amesema kuwa NSSF ifanye mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Nje juu ya
kurejeshwa nchini mmiliki wa Kampuni ya Knight Support Raia wa Uingereza
Bi. Christine Sutton.
Aidha Mhe. Mavunde amesema kuwa Mwakilishi wa Kampuni hapa
nchini Bw.Blessing Kachambwa raia wa Zimbabwe azuiwe kutoka Nchini mpaka
hapo wahusika wakuu wa Kampuni watakaposhughulikia malipo ya
malimbikizo ya michango ya wafanyakazi.Mhe. Mavunde ameeleza kuwa NSSF imeshinda kesi mahakamani juu ya deni hilo tajwa hapo juu na imethibitika kwamba Kampuni ya Knight Support haina mali za kukamata kuuzwa na kufidia deni hilo.
“Kurugenzi ya
Sheria NSSF iandae nyaraka za kisheria za maombi ya kuwakamata wahusika
wakuu na kuwafanya wafunguliwe madai (Civil Prisoners)”, ameelekeza
Mhe. Mavunde.
Pia ameongeza kuwa Mhe. Mavunde ameelekeza kufanyika
Uchunguzi wa kina ufanyike kubaini wafanyakazi wa NSSF ambao
hawakutimiza wajibu wao kwa kutofuatilia michango tangu mwaka 2011-2018.
No comments :
Post a Comment