Mkuu ww wilaya ya Arusha Mjini
Gabriel Daqqaro akizungumza na Vikundi vya Wanawake,Vijana na watu wenye
Ulemavu,ambao hawapo Pichani.
Mmoja wa Mwakilishi wa kundi la
Vijana akiwa ameshika mfano wa hundi katika picha ya pamoja na Viongozi
wa Wilaya na Jiji la Arusha Mjini.
…………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi wetu- Arusha
Halmashauri ya Jiji la Arusha
imekabidhidi Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 626,kwa
vikundi
100 vya Mikopo kwa makundi matatu ya Wanawake,Vijana na watu wenye
Walemavu.
Akikabidhi Hundi hiyo Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alisema fedha hizo ni kutoka Mapato ya
ndani ambapo lengo ni kuwawezesha wananchi, kiuchumi ili kutimiza Sera
ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Daqqaro alisema kuwa serikali ya
Sasa imekuwa ikisisitiza uwekezaji kwenye sekta ya Viwanda hivyo
aliwataka maafisa Maendeleo Kata kuhakikisha kuwa wanatumia elimu yao
vizuri kuvilea vikundi ndani ya kata zao na kuviwezesha kuanzisha
viwanda vidogo vidogo.
“Kwanza niwapongeze kwa
kuhakikisha vikundi hivi vinapatiwa mikopo lakini pia tunataka mikopo
hii ionekane kwa vitendo yaani tuone viwanda vidogo vidogo katika kata
tunaajua nyie mmesoma Sana sasa tumieni elimu yenu kuwasaidia hawa
wananchi kubuni viwanda vidogo vidogo na biashara zinazoonekana.
Aidha alisema kuwa sheria Kali
zitachukuliwa kwa vikundi vitakavyoshindwa kurejesha vizuri mikopo hiyo
huku akivitaka vikundi hivyo kuhakikisha kuwa wanapelekea fedha hizo
kwenye miradi na sio matumizi mengine yasiyotarajiwa.”alisema Daqqaro
“Mikopo hii zamani watu walikuwa
hawazipati lakini kutokana na Rais John magufuli kusema asilimia hii
ipelekwe kwa watu wake ndio maana halmashuri zinatenga na kuwapa
wahusika hao,”alisema Daqqaro
Pia aliwataka Maofisa Maendeleo
Kata kusimamia vizuri vikundi hivyo pamoja na kuelekeza aina za biashara
za kufanya amabazo zitawazalishia fedha badala ya kuvitelekeza.
Ofisa Maendeleo ya Jamii wa
Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mwanamsiu Dossi, alisema fedha hizo
zimetokana na urejeshaji wa zaidi ya Sh.milioni 122.2 wa vikundi
vilivyokopeshwa na zaidi ya Sh.milioni 504.6 zimetokana na fedha za
mapato ya ndani.
Alisema mikopo hiyo iliyotolewa
zaidi ya Sh.milioni 626.8 kati ya hizo Sh.milioni 377 zimetolewa kwa
vikundi 65 vya wanawake,Sh.milioni 234.866 vikundi 32 vya vijana na
Sh.milioni 15 vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa
Halmashuri ya Jiji la Arusha Dk.Maulid Madeni amemwomba Mkuu wa Wilaya
ya Arusha Gabriel Daqarro kuongeza kiwango cha fedha za kukopesha kwa
walengwa hao ili ziwasaidie kufanya biashara.
“Sio lazima tuwapatie fedha
tunaweza kuboresha mikopo hii kwa kununua mfano mashine za kufyatua
matofali,ili kusaidia Vikundi vya vijana lakini pia tunaweza kuwapatia
mashine za kushonea nguo wanawake Hawa wakaweza kujiajiri na pia kuweza
kuzalisha na kupata faida zaidi,ili tuweze kusaidia jamii zetu
vizuri.alisema Madeni
Jumla ya Vikundi 109 viliomba
mikopo hiyo ambapo Vikundi 100,Vimepatiwa mikopo na Tisa vimekosa sifa
huku ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Serikali la kutenga Asilimia kumi
ya Mapato ili kuwasaidia Vijana,Wanawake na Watu wenye Ulemavu.
No comments :
Post a Comment