Washiriki
wa Mafunzo ya Mafunzo ya Haki za Binadamu , unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia hususan kwa wanawake na watoto (wa kwanza kulia) ni Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania, Rehema Kerefu na (wa pili kulia) ni Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Gerald Ndika wakiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.(wa tatu kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Sehel, na (kushoto) ni Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. . Joaquine De Mello na baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa karibu mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakijadiliana kwa pamoja mambo yanayohusu mafunzo hayo.
Na Tawani Salum – Mahakama
Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Jaji Gerald Ndika amewataka
Majaji na Mahakimu kutafsiri sheria zinaohusu masuala ya wanawake na
watoto ili ziendane na mazingira ya sasa katika kuendesha mashauri
yanayohusu masuala la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Akizunguza
wakati wa Mafunzo ya Haki za Binadamu na Unyanyasaji hususani kwa
wanawake na watoto, yanayofanyika Mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani Jaji
Ndika alisema kuwa sheria zilizopo kwa kiwago kikubwa zinajitosheleza
kinachotakiwa jinsi ya kuzitafasiri, hivyo Majaji na Mahakimu watoe
tafsiri ambayo inaendana na mazingira ya matukio yalivyo.
Jaji
Ndika ambaye ni mshiriki katika mafunzo hayo, alisema kuwa moja ya
faida zake ni kuwaandaa wawezeshaji katika eneo hilo ili kusaidia
Mahakama ya Tanzania, Majaji wa Mahakama ya Rufani,Majaji wa Mahakama
Kuu, Mahakimu,watumishi mbalimbali ambao wanatoa maamuzi juu ya vitendo
vya unyanyasaji na ukatili wa wanawake na watoto kuwa na umahiri.
‘‘Matukio
haya yanatokana na mambo mengi ikiwemo mila potofu pamoja na uelewa
wao mdogo, wanaona kumpiga mke au mtoto ni jambo la kawaida na ana haki
ya kufanya hivyo. Lakini ubora wa mafunzo haya yatasaidia kupata
wakufunzi ambao wataenda kuwapa wengine elimu juu ya kuweza kupambana na
ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto,’’ alisisitiza Jaji Ndika.
mafunzo hayo, alisema ni ya mara ya tatu kufanyika yakiwa ni endelevu
katika kutoa elimu hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama
cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) ambaye ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Joaquine De Mello akifungua rasmi mafunzo
hayo, alisema kuwa yana lengo la kuwawezesha watoa maamuzi kuwa na
uweledi zaidi wa kutoa haki na pia kuielimisha jamii juu ya haki zao
za msingi na tatizo la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambalo
limekithiri.
Aliongeza
kwamba kumekuwa taarifa nyingi zinazotolewa na vyombo vya habari pamoja
na wanajamii ambao wamejitokeza wazi kutoa matukio mbalimbali juu ya
suala hilo. Pia tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa hivyo wamegundua
kuwa matukio mengi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia yanafanywa
wahusika wanaotuhumiwa kuwa ni familia au ndugu wa karibu.
Alisema
kuna mapungufu katika jamii kama vile utamaduni wa kutokuwa na utayari
wa kusimamia na kuyapigia kelele tatizo hilo, ikiwa ni sababu
mojawapo ya unyanyasaji na ukatili huo.
‘‘Kupitia
mafunzo haya kama watoa maamuzi tunataka wapate jicho la kipekee shauri
linapokuja mbele yako mara moja unapata picha kuwa hili ni la kikatili
na unalipa nafasi yake na hii itasaidia katika kuandaa taarifa ya
matukio haya kwa usahihi, ikiwemo kuna takwimu ambazo tunazihitaji ili
kujua nguiu gani ya ziada inahitajika katika kusimamia jambo hili,’’
alisema Jaji De Mello.
Mshiriki
mwingine wa mafunzo hayo, ambaye Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Sokoine,iliyopo Jijini Dar es Salaam Mhe, Hanifa Mwingira alisema
jamii inapaswa kuona kuwa vitendo hivyo ni vibaya na kila mtu anapaswa
kusema ‘ukatili sasa basi na mtoto wa mwenzako kuwa ni mtoto wako na
hupaswi kumfanyia ukatili’.
Mwingira
alifafanua kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa viongozi wa dini ambao
watawaelimisha waumini wao, wakiwemo Wenyeviti wa vijiji, kata pamoja
na mitaa na Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Polisi, Magereza na wadau
wengine wa sharia.
Mafunzo
hayo yanayoendelea Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani yalihudhuriwa na Majaji
Wataafu kama vile Mh. Jaji Salum Massati ambaye anashiriki kama mtoa
mada.
Jumla ya washiriki 26 wanapatiwa mafunzo juu ya masuala ya unyanyasaji na ukatili kijinsi. Mafunzo hayo yameanza Juni 27, mwaka huu na yatamalizika Julai Mosi, mwaka huu.
No comments :
Post a Comment