Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Nkasi kuwakamata watumishi watatu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa kula fedha zilizotokana na makusanyo
ya Halmashauri na kujikopesha bila ya kuziwasilisha Benki na hatimae
kuendelea kuibua hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
nchini (CAG).
Mh. Wangabo
ameipa TAKUKURU siku saba kuhakikisha watumishi hao waliokula kiasi cha
Shilingi 27,674,300/= wanarudisha fedha hizo na endapo watashindwa
kufanya hivyo basi wafikishwe mahakamnami haraka iwezekanavyo na kuonya
kuwa wadaiwa wa makusanyo ya halmashauri wamekuwa kama ugonjwa wa
saratani uliokosa dawa huku Mkurugenzi na Madiwani wanaosimamia
halmashauri hiyo wakishindwa kuwawajibisha.
“Nimeambiwa hizi
fedha zinawahusu watumishi wa halmashauri watatu, mmoja anadaiwa milioni
nane, na wengine wawili milioni tisa tisa, imesemwa tu wachukuliwe
hatua za kisheria, lakininhaikutoa muda, hadi lini hawa watu wawe
wamechukuliwa hatua hizo za kisheria, n ahata kwenye maeneo mengi hakuna
muda wa kushughulikia hizi hoja kwamba kufikia tarehe Fulani hii iwe
imekwisha, hakuna, sasa hawa watumishi watatu, TAKUKURU mko hapa, kamata
hawa watumishi watatu, shughulikeni nao haraka iwezekanavyo kuanzia
leo,” Alisema.
Pia ameeleza kuwa
kwa mujibu wa taarifa za CAG kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mapato
yaliyokusanywa bila ya uthibitisho wa kupelekwa benki ni shilingi
47,725,415/= huku shilingi 20,051,115 zikiwa zimerudishwa, lakini
wadaiwa hao hawajirekebishi na matokeo yake taarifa za mfumo wa
ukusanyaji wa mapato hadi tarehe 31, Mei, 2020 unaonesha makusanyo
ambayo hayajapelekwa benki kufikia Shililingi 53,813,308.38/= na hivyo
kuiamrisha TAKUKURU kuwashughulikia.
Mh. Wangabo
ametoa maelekezo hayo leo 3.6.2020 katika kikao cha Baraza la Madiwani
la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuhusu utekelezaji wa hoja za Ukaguzi
na Mapendekezo ya CAG ambapo pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo kuhakikisha analipa madeni ya Madiwani ndani ya siku
saba.
Mh. Wangabo
amechukua hatua hizo ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa maagizo ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Mh.
Suleiman Jafo ambaye hivi karibuni katika ziara yake mjini Sumbawanga
alimtaka Mkuu huyo wa Mkoa kutumia vyombo alivyonavyo kushughulika na
wadaiwa wa fedha za makusanyo ambazo hazikuwasilishwa Benki.
No comments :
Post a Comment