Mkurugenzi Mtendaji wa, Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (katikati) akizunguma na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu ugonjwa wa Corona ulivyo waathiri wafanyabiashara wa sekta isiyo rasmi hasa wanawake. Kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Kitaifa wa Umoja wa Wafanyabiashara Wanawake Masokoni hapa nchini, Betty Mtewele na Mwezeshaji wa Sheria kutoka Shirika la EfG, Aisha Juma ambaye ni Mfanyabiashara wa Tabata Muslim.
Afisa mradi wa EfG , Susan Sitta (katikati) akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI
isiyo ya kiserikali ya Equality for Growth (EfG) imesema
wafanyabiashara wa sekta isiyo rasmi hasa wanawake, wachuuzi wa sokoni
ni miongoni mwa watu walio pata athari za ugonjwa wa COVID 19 .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo, Jane Magigita alisema wafanyabiashara hao kutoka katika
sekta hiyo ni miongoni mwa watu walioathiriwa na Covid-19.
”
Katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa COVID 19 tulitumia nafasi hii
kukusanya maoni ya wanawake kupitia “Vitendawili vya Corona- Simulizi za
wanawake sokoni” ambazo zimetuwezesha kuibua changamoto zinazowapata
wanawake wafanyabiashara zikiwemo kupungua kwa wateja, kushuka kwa
mapato ya biashara, kushindwa kumudu gharama za barakoa na vitakasa
mikono na mazingira kutoruhusu kukaa umbali unaotakiwa katika kujikinga
kutokana na miundombinu masokoni.” alisema Magigita.
Alisema
Covid 19 imekua na madhara makubwa katika ajira hasa katika sekta isiyo
rasmi hivyo kupelekea kuyumba na kuwa ajira imeathirika kutokana na
kupunguzwa kwa masaa ya kufanya kazi, kufanyia kazi nyumbani na hitaji
la kupunguza gharama za uendeshaji.
Alisema
ripoti iliyotolewa na UNDP Tanzania, Economic and Social Research
Foundation (ESRF) imeonyesha madhara ya COVID 19 katika makusanyo ya
kodi, kuongezeka umaskini na utofauti wa kipato kwa Tanzania.
Aliongeza
kuwa ripoti hiyo imekisia madhara makubwa katika sekta ya hoteli na
utalii, uuzaji wa mazao nje ya nchi, usafirishaji na sekta ya fedha pia.
Bila kuwa na hatua madhubuti za kukabiliana na COVID 19 itapelekea
ugumu kuyafikia malengo endelevu ya dunia (SDGs).
Aidha
ripoti nyinginezo nchini zimeonyesha maeneo ambayo yameadhirika sana na
COVID 19 ni pamoja na kupungua kwa idadi ya watalii, mapato ya usafiri
wa ndege, kufungwa kwa biashara karibu na mashule pamoja na vyuo,
biashara za kimataifa, ukwasi wa kifedha, matumizi makubwa kwenye afya,
elimu na wingi wa sintofahamu katika biashara.
Alisema
sekta hiyo inaajiri watu wengi zaidi kwani inatoa ajira kwa takribani
asilimia 90% ya Watanzania na kuwa takwimu zinaonesha katika sekta isiyo
rasmi wanawake ni 74% ya nguvu kazi nchini; 15% ya wanawake pia
wamiliki wa biashara; 54% ni wajasiriamali wadogo na wa kati na kuwa
wako katika nyanja mbalimbali za uzalishaji na mnyororo wa thamani
ikiwemo kilimo, huduma na biashara.
Alisema
EfG imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na jamii na kwa kushirikiana na
Serikali, katika kuwawezesha wanawake wa sekta isiyo rasmi kuwa na sauti
ya pamoja na kuweza kusimamia haki zao za kibiashara na kiuchumi kwa
kupinga ukatili pamoja na vikwazo vya kijinsia.
“Tumewafikia
wanawake kwa kutoa mafunzo ya biashara, uwekezaji, ugawanyaji wa
mapato, kuweka akiba na sera za ujasiriamali. Pia kuwawezesha wanawake
kushika nafasi za uongozi na kushiriki katika nafasi na vyombo vya
maamuzi.” alisema Magigita.
Magigita
alitaja baadhi ya mapendekezo yao juu ya hatua za kuchukuliwa na wadau
mbalimbali kuhusu maendeleo katika majanga ya namna hiyo ni Taasisi za
fedha ziangalie namna bora ya kupunguza makali ya marejesho kwa
wafanyabiashara wadogo na walio katika sekta isiyo rasmi. Kipaumbele
kitolewe kwa wanawake, watu wenye ulemavu, na vijana.
Mapendekezo
mengine ni Taasisi za mbalimbali za fedha zinazotoa mikopo midogo
ambazo hazisimamiwi moja kwa moja na Benki Kuu kama vikundi vya VICOBA,
SACCOS na wakopeshaji binafsi kufikiria namna ya kupunguza riba kubwa
zinazotozwa kwa wafanyabiashara wadogo.
Elimu
ya Ujasiriamali na usimamizi wa fedha itolewe na taasisi mbalimbali kwa
kushirikiana na Halmashauri zote nchini kwa wafanyabiashara ambao wapo
kwenye sekta isiyo rasmi ambao tayari wameathirika na COVID 19.
Kwa
kuwa wafanyabiashara wa sekta isiyo rasmi wengi wao hutumia simu kama
benki, tunashauri wanaotoa huduma za kibenki kupitia mitandao kupunguza
gharama za kutuma na kupokea pesa kutumia mitandao ya simu, na kiwango
cha kutuma pesa kiongezwe.
Halmashauri
zote nchini ziendelee kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana katika
utoaji wa mikopo ya asilimia 10% ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya
miradi na biashara, ambazo zinachangia kumuinua mwanamke kiuchumi.
Benki
Kuu imedhamiria kuziwezesha taasisi za kifedha kuwa na uwezo mkubwa wa
kifedha (ukwasi), ili zitoe mikopo yenye riba nafuu kwa wananchi. Kwa
kufanya hivyo watanzania walio wengi wataweza kukopa kwa riba nafuu
hivyo kuboresha shughuli zao za kuichumi.
Magigita
alisema wanatumia fursa hiyo kuwasilisha mapendekezo kwa
wafanyabiashara ndogo ndogo wa sekta isiyo rasmi waliochukua mikopo
kutoka taasisi za fedha na wameshindwa kuzitumia hizo fedha kutokana na
wateja waliokuwa wanatarajia kuwafikia hawapo tena kutokana na COVID 19,
wasizitumie hizo fedha kwa shughuli mbadala. Wazirudishe kwa mkopeshaji
na wajadiliane kuhusu punguzo la riba.
Biashara
zisibadili matumizi ya fedha wakati huu wa COVID 19, ikibidi kufanya
hivyo basi watafute ushauri kutoka kwa wataalamu au kwa walio
wakopesha/waliowapa fedha.
Wafanyabishara
wawe makini sana katika kutafuta vyanzo vya mitaji katika wakati huu
ili wasije wakaingia katika mitego ya wakopeshaji wenye riba na masharti
yasiyostahimilika.
Kuchangamkia fursa ama unafuu unaotolewa na serikali pamoja na taasisi nyingine wakati huu wa COVID 19 kukuza biashara zao.
Maoni
ya wanawake wafanyabiashara sekta isiyo rasmi masokoni wakitoa maoni
yao kuhusu shughuli zao za kiuchumi kuathiriwa na ugonjwa huo wamesema
kutokana na mapato kupungua sana katika biashara zetu kwani na watu
hawatembelei masokoni na kukaa nyumbani zaidi. Hii imetokana na kupungua
kwa wateja ikiwemo katika mahoteli ambao ndio watumiaji wakubwa wa
mbogamboga na matunda tunayouza sokoni.
Kuwepo
kwa miundo mbinu inayoweza kuimiri majanga, kwani wanawake wengi
waliamua kusimama biashara kwa kuhofia maambukizi ya COVID 19.
Changamoto
ya kushindwa kulipa mikopo kutokana na kipato duni, tunaomba taasisi za
fedha zilizotupa mikopo, ambazo kwa sasa zinapata unafuu kutoka Benki
Kuu zitufikirie zaidi wanawake wa sekta isiyo rasmi.
Sekta
isiyo rasmi tunaomba tufanyiwe tathmini ya athari za COVID 19 na
kuchukua hatua ili kuwezeshwa kwa kupewa mikopo yenye riba nafuu kama
walivyopewa Sekta rasmi nchini.
Wanawake
hao wameipongeza serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa jitihada
kubwa na za kimkakati kuunusuru uchumi hususani wakati wa janga la COVID
19. Sanjari na pongezi zetu tumeamua kama shirika kuunga mkono juhudi
za serikali za kuhakikisha athari za COVID 19 zinapunguzwa kwa kiasi
kikubwa kwa wafanyabiashara wadogo hususani wanawake nchini.
“Kama
alivyosema Raisi wetu Dkt. John Magufuli hivi virusi vinaweza kuwa kama
majanga mengine na tukalazimika kuishi navyo katika maisha yetu yote,
hivyo sera dhabiti zinahitajika kuwasaidia watu wanaoendesha shughuli
zao katika sekta isiyo rasmi waweze kujikwamua. Tunaamini kwa
kushirikiana, nchi yetu itaendelea kuishinda vita dhidi ya COVID 19, na
uchumi wetu kuendelea kuimarika.” alisema Mwenyekiti wa muda wa Kitaifa
wa Umoja wa Wafanyabiashara Wanawake masokoni hapa nchini, Betty
Mtewele.
No comments :
Post a Comment