Msajili wa Baraza la Veterinari
Tanzania Dkt.Bedan Masuruli,akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo
pichani) wakati akitoa taarifa juu ya Afya ya Mifugo nchini pamoja na
kuwataka madaktari kuhuisha majina yao kwenye daftari la usajili wa
madaktari.
……………………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Baraza la
Veterinari nchini limeweka mpango mkakati juu ya kutatu changamoto za
wafugaji ili kuongeza uzalishaji na kuleta tija katika sekta ya ufugaji
nchini.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania Dkt.Bedan
Masuruli, wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma juu ya
kuboresha huduma za ufugaji nchini.
Aidha
Dkt.Masuruli amesema kuwa wamejipanga kusambaza wataalamu wa mifungo
ngazi za msingi ili kuwa karibu na wananchi na kuwashauri namna ya
kuipatia kinga mifugo hiyo na kuleta tija katika ufugaji wao.
Dkt.Masuruli amesema kuwa ili
kufikia adhima hiyo amesema kuwa lazima wataalamu wote wa ngazi ya
msingi kusajiliwa, kujiandikisha na kujiorodhesha katika daftari ili
kusaidia wizara ya mifugo kujua ubora wa wataalamu walionao katika
maeneo ya kusaidia wananchi katika kuongeza tija sekat ya ufugaji.
Aidha
Dkt.Masuruli amesema kuwa wameongeza muda kwa wataalum kuhuisha majina
yao kwenye daftari la usajili wa madaktari kabla ya tarehe 1 julai mwaka
huu wawe tayari wamejisajili
“ Baada ya
kuhuisha taarifa zao hao wataalamu watapatiwa vitambulisho maalum ili
kusaidia wafugaji na wananchi kutambua kuwa ni mtaalamu aliyekidhi
viwango hivyo mwananchi anaweza patiwa huduma kwa kupata ushauri, kinga
na namna ya kuboresha ufugaji ili kufikia mafaniko makubwa”,
Dkt.Masuruli
Dkt.Masuruli
amesema kuwa Wataalamu hao katika maeneo yao watatakiwa kuwasilisha
taarifa za wafugaji wizarani ili kusaidia serikali kuandaa mpango kazi
wa kutatua changamoto zilizoshindikana kutatuliwa na wataalaum hao.
Hata hivyo
Dkt.Masuruli amesema kuwa Lengo kuu la kusogeza huduma hizi kwa wananchi
ni kutaka kuhakikisha wanapatiwa huduma bora zinazokidhi viwango na
itasaidia kubaini magonjwa yanayojitokeza katika mifungo ya wanachi
wanao wahudumia na kuwasaidia kwa ukaribu.
“ Natoa wito kwa
vituo vyote vya afya ya wanyama kuanzia Julai Mosi Mwaka huu kuweka
mpango wa muda wa miezi mitatu kupata hadubini katika vituo hivyo ili
kusaidia kujua magonjwa katika mifugo ya wanachi wao wanao wahudumia”,
amesema Dkt.Masuruli
Dkt.Masuruli ameongezea kuwa
wananchi kupata na kunufaika na ufugaji wanahitaji wataalamu wa mifugo
kuwa karibu na wafugaji ili kuwasaidia kuwapatia huduma bora
itakayokidhi viwango na kuleta tija kwa asilimia kubwa na kuinua kipato
cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment