***************************
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Gerald Mweli amesema asilimi 90 ya
wanafunzi wa kidato cha sita wameripoti shuleni katika halmashauri
zote
nchini.
Pia amsema mpaka sasa hakuna
taarifa yoyote ya kuwapo maambuziki ya ugonjwa wa Corona kwa wanafunzi
wa kidato cha sita walioripoti shuleni.
Akitoa tathimini ya uripotiji wa wanafunzi shule ambao walitakiwa kuanza masomo Juni 1 mwaka huu, Mweli alisema
Alisema wanafunzi hao wameanza
masomo yao majuzi na kuwa leo wataanza kufanya mitihani ya majaribio ili
kufanya tathimini ya maeneo ambayo wanafunzi yanawasumbua.
Aidha, Mweli alisema mpaka hakuna taarifa ya kuwapo mwanafunzi mwenye dalili za kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
“ Napenada niwatoe hofu wazazi
kuwa watoto wanaafya njema na kuanzia jana na leo (juzi na jana) hatuna
tukio au taarifa ya kuwapo mwanafunzi yeyote mwenye dalilia za kuwa
ameambukizwa ugonjwa wa Corona.
Mweli pia alisema katika shule
zote kumekuwapo maandalizi mazuri ya kuwapokea wanafunzi na kuwa shule
zote zimezingatia mwongozo uliotolewa na wizara ya afya.
“ Tumejipanga kuwa na maji ya
kutosha, sabuni za kutosha katika shule zetu na kuzingatia suala la
umbali wa mwanafunzi mmoja na mwingine ili kuwafanya wanafunzi wetu kuwa
salama.”
Mweli aliongeza: “ Nimategemeo
yetu kuwa ndani ya wiki mbili kutoka sasa wale wanafunzi ambao watakuwa
wamefanya mitihani ya majaribio watakuwa wamesahihishiwa na kubaini
maeneyo yenye upungufu
Alisema Tamisemi imeandaa program maalumu ya kuhakikisha topiki ambapo zimewatatizia wanafunzi zinafanyiwa marejeo
“ Nitoe wito kwa walimu na wakuu
wa shule kuwa mipango tuliojiwekea na hali inavyokwenda sasa tuhakikishe
tunasimamia na tunakuwa karibu na watoto na kuzungumza nao mara kwa
mara na kuzidi kuwapa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Aidha, Mweli aliwataka walimu,
wakuu wa shule na mameneja wa shule binafasi kuhakikisha wanatekeleza
katazo la kuwataka wanafunzi kwenda shule na tangawizi, malimao.
“ Tulizuia wanafunzi kwenda na
limao na tangawizi, hivyo hakuna sababu ya kuufanya mwanafunzi kushindwa
kurudi shuleni kwa sababu hiyo.
“ Nitoe wito kwa walimu, wakuu wa
shule na mameneja wa shule binafasi kuhakikisha wanazingatia maelekezo
ya serikali kuhuzu zuio la kuwataka wanafunzi kwenda na tangawizi, limao
au spiriti ambayo yalikatazwa.
Aidha, Mweli alitumia fursa hiyo
kuwasisitiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha
wanasimamaia kwa karibu shule zilizo maeneleo yao ili kuhakikisha watoto
wanakuwa salama mpaka hapo watakapomaliza mitihani yao ya kidato cha
sita.
Pia amwataka walimu, wakuu wa
shule na mameneja wa shule binafsi wametakiwa kutekeleza mwongozo wa
wizara ya afya uliotolewa na serikali na kuwa hawatasita kumchukulia
hatua mtu yeyote anayekwenda kinyume na mwongozo na maelekezo ya shule.
Hivi karibuni, Rais John Magufuli
alitangaza kufunguliwa kwa vyuo na wanafunzi wa kidato cha sita baada ya
maambukizi ya ugonjwa wa Corona kuzidi kupingua ikiwa imepita miezi
kadhaa ya kufungua shule na vyuo kutokana na kuwapo kwa maambukizi ya
ugonjwa huo.
No comments :
Post a Comment