Sunday, May 31, 2020

Matukio mbalimbali duniani wiki hii – Picha


Mwanamke aliyekutwa amebeba mizigo na mtoto wake akielekea katika moja ya kambi duni iliyopo Faladie mjini Bamako, Mali juzi. (Picha na AFP).Watu wakiwa katika mstari kuelekea kupokea chakula cha bure kinachotolewa na Serikali mjini Bangkok, Thailand ili kuwapunguzia gharama za maisha wananchi kipindi hiki cha mlipuko wa corona. (Picha na REUTERS)Afisa wa Jeshi la Polisi nchini Indonesia akinyunyizia dawa pikipiki katika kituo cha ukaguzi kilichopo Surabaya Aprili 28, mwaka huu. Mkakati huu unalenga kudhibiti virusi vya corona katika vyombo vyote vya moto na mizigo. (Picha na AFP).Baadhi ya maafisa wa Kikosi cha Uokoaji na Zimamoto nchini Korea Kusini wakishirikiana kuzima moto katika ghala la kuhifadhia bidhaa lililokuwa linateketea juzi mjini Icheon. Katika ajali hiyo zaidi ya watu 38 waliripotiwa kufariki na mamia kujeruhiwa. (Picha na AFP).Kikosi cha Bandari nchini Ufilipino kikisambamza baadhi ya bidhaa na chakula kwa wananchi waishio katika Pwani ya Manila Bay Aprili 27, mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kuwasaidia kumudu maisha kipindi hiki. (Picha na EPA-EFE).MA Bibi na Bwana wakishiriki mlo wa usiku katika moja ya migahawa jijini Paris, Ufaransa jana huku wakiwa wamechukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona (COVID-19) kwa kuvaa ngao maalum za plastiki. Ripoti zinaonyesha kuwa, ugonjwa wa Corona bado upo na unaendelea kusambaa kwa kasi, hivyo ni jukumu la kila mmoja kuchukua tahadhari. (Picha na AP).Mwanaume aliyekutwa akipita kwenye maji mengi yaliyosababisha mafuriko makubwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Mei 26, mwaka huu mjini Miami nchini Marekani na ku.(Picha na AFP).Mkulima raia wa Nepal akivuna ngano katika mji wa Bhaktapur juzi, wakulima wengi wameshauriwa kuweka akiba ya chakula kutokana na mwenendo usioridhisha wa hali ya hewa Duniani, hivyo kuwepo hofu ya baa la njaa. (Picha na AP).Watu kutoka kaya maskini mjini Puete Alto, Santiago nchini China wakifanya maandamano kuishinikiza Serikali kuwapatia chakula baada ya kuwaweka ndani ikiwa ni hatua ya kujiadhari dhidi ya virusi vya Corona Mei 25, mwaka huu. (Picha na REUTERS).

No comments :

Post a Comment