Jeshi
la polisi mkoa wa Arusha baada ya kupata taaarifa fiche limefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wanne wa ujambazi akiwemo Mganga wa Kienyeji
wakiwa na silaha mbili za Moto kwa ajili ya kuja kufanya matukio ya
kiuhalifu mkoani hapa.
Akizungumza
na vyombo vya habari mkoani hapa kamanda wa polisi Jonathan Shana
amesema jeshi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao ni Steven Godfrey
(32) mkazi wa Tabata, Yunusi Hamed (37)mkazi wa Tanga, Said Hamisi(38)
mkoa Dar es salaam na mwingine Msafiri Yohana (22) mkazi wa mwanza.
Mnamo
tarehe 6 mwezi wa tano meaka huu majira ya saa nne usiku huku maeneo ya
daraja la Nduruma Kata ya Baraa Halmashauri ya jiji la Arusha jeshi
letu lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne wa Ujambazi waliokutwa na
bunduki moja na Bastola moja zenye jumla ya Risasi 12 .
Alisema
mnamo majira ya saa nne baada ya kupata taarifa fiche ambapo tuliweka
mtego maeneo ya daraja la mto turuma ndipo tulipowaona watuhumiwa hao
waliotekea Dar es salaam kuja Arusha kwa kutumia gari aina ya Toyota
crown, lenye namba la usajiri T. 777 DSJ ndipo walipolisimamisha gari
hilo lakini walikaidi amri.
Hata
hivyo askari walichukua uamuzi wa kufyatua risasi hewani kwa lengo la
kuwataadharisha lakini waliendelea kukaidi amri hiyo, ndipo Askari
walipoamua kufyatua risasi kwa kulenga matairi ya gari hilo hali
iliyosababisha kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao huku mmoja wao
aitwaye Msafiri Yohana akiwa amejeruhiwa kwa risasi katika viganja vyake
vya mikono.
Aidha
kwa mujibu wa Kamanda Shana katika upekuzi wa gari hilo kulikutwa na
aina za silaha mbili Shortgun (1) na bastola 1 zenye risasi nne za
bunduki aina ya Shortgun na risasi nane za bastola zilizokuwa kwenye
magazine pamoja na mikasi mitatu ya kukatia vyuma, nondo mbili, gundi na
madawa mbalimbali ya mitishamba.
Alieleza
Kamanda katika mahojiano na watuhumiwa hao wamekiri kuja Arusha kwa
leongo la kufanya uhalifu na watuhumiwa hao watafikishwa mahakani pindi
upelelezi utakapokamilika, ambapo akatoa wito kwa watu wote wenye nia ya
kufanya uhalifu awatafanikiwa kuingia lakini watatoka majivu.
Pia
niwaombe wananchi waendelee kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu
kwa jeshi hilo ili waweze kuzifanyia kazi hali itakayosaidia kuimarisha
utulivu, amani na usalama tulivu uliyopo.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha alilipongeza jeshi hilo kwa kufanya
kazi zake kwa weledi na kuwataka wananchi kufuata Maelekezo ya kutii
sheria bila shuruti na wanaoshindwa mmekuwa mkiwashurutisha kama hawa
Alisema
kuwa kila wakati jeshi hilo limekuwa likiwataka wananchi kutiii sheria
bila shuruti na wanaokaidi mmekuwa mkiwashurutisha leo mmenyesha mfano
mmekamata majambazi wametii sheria na hawakuu wawa na matokeo yake ni
tofauti na huko nyuma wengi walikuwa wakikaidi na kujikuta wakiuwawa.
No comments :
Post a Comment