*****************************
Na Emmanuel Shilatu
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mbunge wa Iramba Magharibi) kuwa Waziri wa
Katiba na Sheria. Hafla iliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita , Mei
03, 2020. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi ya Balozi Dkt.
Augustine Philip Mahiga aliyefariki dunia tarehe 01 Mei, 2020.
Baadhi ya Watu
wanasema Rais Magufuli amedanganya juu ya upimaji wa Papai kwa sababu
Papai halina damu! Watu hawa wanashindwa kuelewa sampuli za upimaji wa
virusi vya Corona ni za maji maji mfano mate, makamasi na si damu. Watu
hawa “vilaza” wanaodai Rais amepotosha wanataka kutuaminisha Papai
halina majimaji yatakayoweza kutumika kama sampuli ya upimaji?
Wengine wanasema Rais
Magufuli hajui tatizo wala ukubwa wa Corona nchini. Watu hawa
wanashindwa kuelewa Urais ni taasisi ambapo yeye anapokea taarifa yeyote
ile anayoitaka muda wowote ule.
Rais huyu wanayemsema
hajui tatizo la Corona nchini ndio Rais huyu huyu alisitisha zoezi la
uwashaji Mwenge, maadhimisho ya sherehe za Muungano na maadhimisho ya
sherehe za Wafanyakazi na kuelekeza fedha hizo ziende kupambana na
ugonjwa wa Covid 19. Huu ni ushahidi tosha kuwa analitambua tatizo
lilivyo na ukubwa wake.
Ni katika Serikali
yake ametoa maelekezo ya Kiserikali ya kufunga shule za msingi na vyuo;
kusitisha michezo yote nchini; kutoa maelekezo wageni wote wanaoingia
nchini wawekwe karantini kwa siku 14. Hizi zote ni baadhi ya jitihada za
Serikali kutambua tatizo na harakati katika kupambana na tatizo la
virusi vya Corona nchini.
Wengineo baadhi
wanasema Rais Magufuli amekimbia tatizo kwa kwenda kujichimbia kijijini
kwao Chato. Watu hawa wanasahau ya kuwa Rais hana mipaka ya ukaaji,
mipaka ya kufanya kazi kijiografia na ndio maana hata tatizo la ugonjwa
wa Corona aliliweka wazi akiwa barabarani kwenye ziara ya ukaguzi wa
ujenzi wa Ubungo interchange na wala hakuwa ofisini ama Ikulu na
utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa barabarani ya kukabiliana na tatizo
yakaanza mara moja. Hiyo ndio nguvu na mamlaka ya Rais neno lake
analotamka hata kama akiwa uchochoroni ni agizo la kufanyiwa kazi mara
moja.
Ni Rais Magufuli huyu
huyu ambaye hatujawahi kusikia akisafiri safiri nje ya nchi amebaki
ndani akikabiliana vyema na matatizo ya ujambazi, mauaji ya Kibiti,
Panyaroad na hadi sasa imebaki historia na tatizo kuisha. Rais Magufuli
ameyaweza magumu yote hayo yakiwemo ya ufisadi nchini hata hili la
Corona nalo pia amelimudu na tatizo litaweza kuisha endapo
tutashirikiana kwa pamoja.
Ndugu zangu, ni
jukumu letu sote kuhakikisha tunashikamana kwa pamoja kuhakikisha
tunapambana vilivyo na adui Covid 19 kwa kuhakikisha tunaepuka
mikusanyiko, hatushikani mikono, tunavaa barakoa, tunanawa mikono mara
kwa mara kwa sabuni na maji yanayotiririka na si kuweka pembeni
maelekezo ya Wataalamu wa afya na kuchukulia suala hili kisiasa,
hatumkomoi Rais Magufuli bali tunajikomoa sisi wenyewe na jamii yetu.
Hatuwezi kupambana na
ugonjwa huu kwa kuchafuana, kutishana na kutiana hofu. Ni wakati wa
kusimama imara tusijiyumbishe kwani hili litapita kama yalivyopita
mengine.
Tuache kupeana hofu,
tumeishinda hii vita tayari kwani Serikali ya Rais Magufuli imepambana
vilivyo na tatizo hili na si kubwa kulinganisha na nchi nyinginezo
lilivyo.
Narudia tena kusema
tumeishinda hii vita tayari, tuungane kwa pamoja kukabiliana na tatizo.
Tusimame na Rais Magufuli, tusimame na ukweli. Vita tumeishinda,
tutavuka salama daraja.
No comments :
Post a Comment