Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa Bi. Stephanie Mouen Essombe,
wakisaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Euro milioni 70 (Sh.
za Tanzania bilioni 175.6) kwa ajili ya kugharamia mradi wa Maji Safi
na Usafi wa Mazingira mjini Morogoro (MORUWASA), jijini Dodoma. Anaye
waongoza ni Mwanasheria wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Nyanzala
Nkinga
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe,
wakibadilishana hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Euro
milioni 70 (Sh. za Tanzania bilioni 175.6) kwa ajili ya kugharamia mradi
wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Morogoro (MORUWASA), jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati) akiwa na Katibu
Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ) Bi. Stephanie Mouen
Essombe wakati wa hafla ya kusainiwa kwa mkataba wenye masharti nafuu
ambapo AFD imeikopesha Tanzania Euro milioni 70 sawa na shilingi za
Tanzania bilioni 175.6 kwa ajili ya Mradi wa Maji safi na Usafi wa
Mazingira Mjini Morogoro (MORUWASA).
Meza kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James (katikati), kulia kwake
ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Tanzania Bi.
Stephanie Mouen Essombe na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji
Prof. Kitila Mkumbo ikiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara
ya Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya Serikali ya
Tanzania na Ufaransa kutiliana Saini makubaliano ya mkopo wa masharti
nafuu wa Euro milioni 70, Jijini Dodoma.

Meza kuu
ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James
(katikati), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la
Ufaransa, Tanzania Bi. Stephanie Mouen Essombe na kushoto kwake ni
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo ikiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maji akiwemo naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Eng. Antony Sanga (wa pili kushoto mstari wa nyuma) pamoja na
wafanyakazi wa mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingra Mjini Morogoro
(MORUWASA) mara baada ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa kutiliana
Saini makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu wa Euro milioni 70, Jijini
Dodoma.

Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James akizungumza na wanahabari
(hawamo pichani) mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti
nafuu wa Euro milioni 70, sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 175.6
kati ya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa ajili ya Mradi wa
Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Morogoro (MORUWASA), katika hafla
iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mkoani Morogoro Eng. Tamim
Katakweba akieleza namna mkoa wa Morogoro ulivyojipanga kutekeleza mradi
wa maji safi na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Morogoro baada ya Serikali
ya Tanzania na Ufaransa kutiliana Saini makubaliano ya mkopo wenye
masharti nafuu wa Euro milioni 70 kwa ajili ya mradi huo utakao
wanufaisha zaidi ya wakazi 722,000 wa Mji wa Morogoro, tukio hilo
limefanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Maji Eng. Sanga (Katikati), Mkurugenzi wa Fedha za Nje Wizara
ya Fedha na Mipango Bi. Sauda Msemo na Afisa Mwandamizi wa Idara ya
Fedha za Nje Bw. Mbise (walioketi viti vya mbele) pamoja na maafisa
wengine wa Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa
makini tukio la utiaji saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa
Euro milioni 70, uliotolewa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD)
kwa ajili ya kugharamia mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini
Morogoro (MORUWASA), jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Bi. Stephanie Mouen Essombe,
wakionesha hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Euro
milioni 70 (Sh. za Tanzania bilioni 175.6) kwa ajili ya kugharamia mradi
wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Morogoro (MORUWASA), jijini
Dodoma.
(Picha na Saidina Msangi – Wizara ya Fedha na Mipango)
**********************************
Na Farida Ramadhani-WFM, Dodoma
Serikali ya
Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetiliana saini
mkataba wa
mkopo wenye masharti nafuu wa Euro milioni 70, sawa na
takriban shilingi za Tanzania bilioni 175.6 kwa ajili ya kugharamia
Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazigira Mjini Morogoro (MORUWASA).
Mkataba wa
mkopo huo umesainiwa Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James kwa upande wa Serikali na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Bi. Stephanie Mouen Essombe.
Bw. James alisema
mkopo huo utawezesha wakazi wa Mjini Morogoro wapatao 722,010 kupata
maji safi na salama kupitia upanuzi wa mfumo wa usambazaji wa
Maji kutoka Bwawa la Mindu.
Alisema
kukamilika kwa mradi huo kutawezesha upatikanaji wa Maji kutoka mita za
ujazo 33,000 hadi kufikia mita za ujazo 108,000 kwa siku pamoja na
kuwezesha Mji wa Morogoro kupata kiwango cha mahitaji ya maji safi
kinachokadiriwa kuwa mita za ujazo 126,253 kwa siku, ifikapo mwaka 2035.
“Mradi pia
utaongeza upatikanaji wa huduma za majitaka kutoka kiwango cha sasa cha
asilimia 5 hadi asilimia 15 kwa wakazi wa mjini Morogoro”, alifafanua.
Bw. James
alisema Tanzania imekuwa ikinufaika na ufadhili wa AFD hususan katika
sekta za Nishati, Maji, Usafirishaji na Kilimo kupitia idadi ya miradi
mbalimbali inayoendelea na ile inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Alisema miradi
7 inayoendelea kutekelezwa katika sekta mbalimbali hapa nchini kupitia
misaada na mikopo inayotolewa wa Shirika hilo inafikia takriban Euro
milioni 154.5 sawa na shilingi bilioni 387.6.
“Miradi 6
yenye thamani ya Euro milioni 141.4 kupitia ufadhili wa AFD imekamilika
na kuna miradi mingine 12 yenye thamani ya Euro milioni 1,021.7 ambayo
tuko kwenye mazungumzo na AFD katika sekta ya Nishati, Maji, Kilimo
Usafiri wa mwendokasi Jijini Dar es Salaam, miundombinu ya viwanja vya
ndege na Usafi wa mazingira Jijini Dare salaam” alisema Bw. James.
Aliishukuru Serikali
ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa ufadhili
huo muhimu, ambao utachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi na
kupunguza umaskini na kuahidi kuwa Serikali itafuatilia kwa karibu
utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha kwamba fedha zitakazotolewa
zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Bi.
Stephanie Mouen Essombe aliahidi kuwa shirika hilo litaendelea
kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha inafikia malengo
yake katika kuboresha maisha ya wananchi hasa katika upatikanaji wa
maji.
“Ushirikiano wa
Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ulioanza miaka 20
iliyopita umezidi kuimarika ambapo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita
Shirika limewekeza kiasi cha Euro milioni 258 sawa na takriban Sh.
bilioni za Tanzania 655” alisema Bi. Essombe.
Alisema mradi huo
umelenga kupanua Bwawa la Mindu linalochangia upatikanaji wa maji
yanayotumika katika Mji wa Morogoro kwa asilimia 70 pamoja na kuboresha
mfumo wa huduma ya maji taka katika mji huo.
Naye Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo alisema kuwa mkopo huo utatatua
changamoto ya maji ambayo ilikuwa kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa
Morogoro.
Alisema mkopo huu
unafaida nyingi nchini ikiwemo kutoa ajira pamoja na kutoa fursa kwa
viwanda vya ndani kwa sababu vifaa vitakavyotumika kutekeleza mradi huo
wa kihistoria vitanunuliwa ndani ya nchi.
Alisema hivi sasa
Serikali inatekeleza miradi ya maji 1,423, miradi 792 imekamilika na
miradi 631 inaendelea na kwamba mradi huo wa maji wa Mji wa Morogoro
utakuwa mkombozi mkubwa wa wananchi wa mji huo.
Alisema
upatikanaji wa fedha hizo ambazo mjadala wa kupata mkopo umechukua zaidi
ya miaka minne utawezesha kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji
nchini ambapo hivi sasa kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini
kimefikia asilimia 85 ya lengo la asilimia 95 iliyoainishwa katika Ilani
ya Uchaguzi ya CCM huku katika miji kiwango kimefikia asilimia 70.1
kati ya lengo la asilimia 85 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020
No comments :
Post a Comment