Hospitali na vituo vya afya vinapambana kuongeza nguvu kazi katika sekta ya afya katika kukabiliana na janga la corona.
Hitaji la watoa huduma za
afya limekuwa kubwa kufuatia idadi kubwa ya waathirika wa virusi vya
corona kwenye hospitali na vituo vya afya.
Mchango wa kila mmoja katika sekta ya afya unahitajika katika kuhakikisha nchi inapita salama katika kipindi hiki kigumu.
Baadhi ya nchi zimekwenda mbali
kwa kuwarudisha madaktari wastaafu na hata kuwatumia walikuwa katika
mwaka wa mwisho wa kuhitimu ili kukabiliana na upungufu wa watoa huduma
za afya.
Kwa upande wa Tanzania hivi
karibuni ajira 6000 za madaktari zilitangazwa kwa lengo la kuongeza
nguvu katika mapambano dhidi ya corona.
Kama moja ya jukwaa la huduma za
rasilimali watu nchini Tanzania, BrighterMonday Tanzania imechukua
hatua kadhaa kuhakikisha sekta ya afya inaendelea kuwa na wataalamu wa
kutosha kusaidia mapambano dhidi ya janga la corona.
“Tunaelewa kwamba mamilioni ya
wafanyakazi ulimwenguni kote wameathiriwa na mlipuko wa COVID-19. Sekta
ya afya imeathiriwa zaidi na janga hili. Hii ndiyo sababu BrighterMonday
Tanzania tumeendelea kutoa mchango wetu wa hali na mali kwa sekta ya
afya na sekta nyingine zote zilizopo mstari wa mbele katika mapambano
dhidi ya coroa.
Moja ya hatua muhimu ni
kuanzisha programu ya Umoja Wakati wa Shida ambayo inawapa waajiri
nafasi ya kutumia jukwaa letu bure na kupata huduma muhimu za rasilimali
watu kwa punguzo kubwa”, anasema Reshma Bharmal-Shariff, Mkurugenzi
Mkuu wa BrighterMonday Tanzania.
“Huu sio wakati ambao sekta ya
afya inapaswa kuhofia suala la kupata nguvu kazi. Nguvu na akili zao
zinapaswa kuelekezwa katika kupambana na janga la corona wakati
tukiwasaidia kupata ‘askari’ sahihi watakaoongeza nguvu katika
mapambano. Kwa kutumia teknolojia ya Best Match waajiri wanaweza kuajiri
kwa ufasaha na kwa muda sahihi”, ameongeza Reshma.
Kwa kutumia teknolojia ya Best
Match, wataalamu wa afya wenye uwezo na wanaoendana na mahitaji
watachanguliwa kulingana na nafasi husika na watapewa kipaumbele katika
mfumo ili kupunguza usumbufu kwa waajiri.
“Matumizi ya teknolojia ya Best
Match yatapunguza usumbufu kwa waajiri ambao walipaswa kutumia muda
mwingi kuchagua wataalamu ambao wanafaa kutokana na nafasi husika.
Waajiri wanaweza kutumia muda huo kufanya majukumu muhimu ya kupambana
na janga la corona wakati BrighterMonday tukiwasaidia kupata wataalamu
sahihi. BrighterMonday Tanzania itawasaidia waajiri kupata walau
wataalamu 10 katika siku saba za kuweka tangazo la ajira”, amesema
Reshma.
No comments :
Post a Comment