Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Mama
Anne Makinda akizindua mpango wa Machinga Afya unaotoa fursa kwa
machinga kujiunga na huduma za matibabu kwa gharama nafuu.
Sehemu ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF.
Mwanachama kupitia mpango wa Machinga Afya akifuarahia baada ya kupokea kadi yake ya matibabu.
Mama Anne Makinda akikabidhi kadi kwa wanachama wapya kupitia mpango wa Machinga Afya.
Mwenyekiti wa Bodi Mama Anne
Makinda akishuhudia uwekaji wa Saini wa Mkataba wa Makubaliano ya huduma
hiyo kati ya Machinga na NHIF

Zoezi la utiaji wa saini likiendelea.
……………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
WAMACHINGA nchini wamesema kuwa,
kitendo cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kukamilisha na kuzindua rasmi
mpango wa huduma za matibabu kwa kundi hilo unaojulikana
kama Machinga
Afya ni kuwakomboa kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
Wamachinga Tanzania Bw. Stephen Lusinde, Dar es Salaam leo wakati wa
uzinduzi wa mpango huo ulioambatana na kusaini mkataba wa makubaliano
kati ya Mfuko na Chama cha Wamachinga wa namna ya uendeshaji wa huduma
kwa kundi hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo,
amesema kwamba kitendo cha kuzinduliwa kwa mpango huo ni sawa na
Machinga kuzaliwa upya wakiwa na matumaini ya ulinzi wa afya zao na
uchumi wao.
“Hakika siku ya leo kwetu ni sawa
na kuzaliwa upya, hapo awali hatukuwa na uhakika wowote wa ulinzi wa
afya zetu, kupewa fursa hii na Mfuko inatuhakikishia usalama zaidi wa
mitaji yetu lakini uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote,”
alisem Bw. Lusinde.
Alitumia fursa hiyo kutoa pongezi
zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa namna ambavyo amehakikisha chini ya uongozi wake kunakuwa
na uhakika wa huduma zote za kijamii ikiwemo suala la afya ambalo ni
suala nyeti.
“Miaka ya nyuma sisi tulijiona
kama ni kundi ambalo limetengwa lakini kwa kitendo hiki cha sisi kuanza
kutumia huduma za NHIF sasa tunatembea kifua mbele na katika hili naomba
niwapongeze sana Mfuko kwa kuhakikisha hili linafanikiwa na Wamachinga
wote nchini wamepokea hili kwa furaha kubwa,” alisema Bw. Lusinde.
Akizindua mpango huo, Mwenyekiti
wa Bodi ya NHIF, Mama Anne Makinda alisema kuwa tendo la uzinduzi huo ni
matokeo chanya ya kazi kubwa iliyofanywa kuhakisha kila kundi la
wananchi linakuwa na fursa ya kujiunga na huduma za matibabu.
Alisema kuwa kauli ya HAPA KAZI TU iliyotolewa
mwaka 2015 na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli imekuwa na matokeo makubwa
sana ambayo kila mmoja kwa sasa anaweza kuyaona kwa macho.
Alisema kuwa Serikali imefanya
kazi kubwa ya uboreshaji wa hospitali nchini na huduma za matibabu kwa
ujumla hatua inayowezesha upatikanaji wa huduma zote za matibabu
kirahisi na kuondoa changamoto zilizokuwepo awali zikiwemo za ukosefu wa
dawa.
“Mfuko umejipanga sana
kuwahudumia wananchi na kuwafikia katika maeneo yao, hivyo natoa wito
kwa watoa huduma kuhakikisha wanawahudumia wanachama kulingana na
maadili yao ya kazi,” alisema Mama Makinda.
Aidha aliwaomba wananchi kuwa na
kipaumbele katika kuwekeza kwenye afya zao badala ya kuelekeza fedha
katika mambo mengine kama ya kuchangia harusi na sherehe zingine.
Akielezea namna Mfuko
ulivyojipanga kutoa huduma kwa kundi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.
Bernard Konga amesema mkakati uliopo ni kutoa huduma bora kwa wanachama
na kuendelea kuwafikia wananchi ili waweze kujiunga.
“Leo tunaanza na kundi la
Wamachinga wa Kariakoo ambao wana utaratibu mzuri sana wa kuratibu
wanachama wao na mpango huu umelenga kuwawezesha wajasiliamali hawa kwa
gharama ya shilingi 100,000 tu kwa mwaka hivyo niwahakikishie kuwa
upatikanaji wa huduma ni wa uhakika kabisa,” alisema Bw. Konga.
No comments :
Post a Comment