Watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walio tumia fedha za makusanyo ya
ndani kiasi cha shilingi milioni 22.083 wametakiwa kuzirudisha ndani ya
siku tatu huku Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU
ikielekezwa kusimamia hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa agizo hilo
wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje
la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG).
Brig.
Jen, Mwangela amesema hakuna mtumishi au mtu yeyote atakayetumia fedha
za Serikali kwa Mkoa wa Songwe akabaki salama hivyo wote wanaodaiwa
kukusanya mapato ya ndani na kuyatumia waziridishe au wakamatwe hadi
watakapo zirudisha fedha hizo.
Amesema
TAKUKURU hawapaswi kucheka na wala fedha za serikali kwakuwa madiwani
wanahangaika kwa kushirikiana na serikali kubuni vyanzo vya mapato ili
fedha hizo zitakazo kusanywa ziboreshe huduma za jamii na kukuza uchumi
hvyo wanaozitumia hawapaswi kuvumiliwa.
Brig.
Jen Mwangela ameongeza kuwa katika taarifa ya CAG Halmashauri ya Wilaya
Ileje imepata hati yenye mashaka katika kuzingatia taratibu na sheria
za manunuzi hivyo Mkurugenzi ahakikishe wataalamu wake wanafuata sheria
na taratibu za Manunuzi pia madiwani wahahakishe wana simamia watumishi
wasikiuke taratibu hizo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji
Mnasi amemshukuru Mkuu Wa Mkoa wa Songwe kwa kushiriki kikao hicho na
kuahidi kuwasimamia watumishi wafuate taratibu na sheria.
No comments :
Post a Comment