Na Masanja Mabula , Pemba.
JESHI la Polisi
Mkoa wa Kaskazini Pemba linajipanga kuiandikia barua wizara ya
mawasiliano ili kuomba wafutiwe leseni madereva wazembe wanaosababisha
vifo.
Kauli ilitolewa na
Kamanda wa Polisi Mkoa huo , Kamishna Msaidizi Mwandamizi Juma Sadi
Khamis wakati akizungumza kufuatia kutokea ajali iliyosababisha kifo cha
mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.
Alisema jeshi la
Polisi limekuwa likitoa taaluma kwa madereva kuheshimu sheria za
usalama barabarani, lengo ni kuwataka kufuata sheria ili kunusuru
maisha ya abiria wasio na hatia.
“Tumeona njia
sahihi ya kukabiliana na ajali ni kuwafutia leseni madereva wazembe
wanaosababisha vifo na ulemavu kwa baadhi ya wananchi”alieleza.
Hivyo Kamanda wa
Sadi aliwataka madereva kusimamia na kufauata sheria bila ya
kushurtishwa lengo ni kulinda uhai na maisha ya watu.
Kamanda Sadi
aliyasema hayo baada ya gari ya mizigo aina ya HINO yenye namba za
usaliji Z 301 HJ iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Amour Saleh Seif kuacha
njia na kupinduka na kusabisha kifo cha mtu mmoja mkaazi wa Micheweni
Pemba.
Aliyefariki
kutokana na ajali hiyo ni Mahadi Subeti Khamis 20 ambapo waliojeruhiwa
na kulazwa hospitali ya Micheweni ni Ali Dawa Faki 18, Faki Dawa Faki 32
na Ali Suleiman Ali 34.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Kaskazini Pemba kamishna Msaidizi Mwandamizi Juma Sadi Khamis
alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Kamanda Sadi
alisema ajali hiyo ilitokea mei 28 majira ya saa tatu na robo , ambapo
dereva huyo gari ilimshinda na kuacha njia na kupinduka.
“Uchunguzi wa
awali ilibaini kwamba chanzo cha ajali hio ni mwendo kasi kwani dereva
ilimshinda gari na kuacha njia na kupinduka na hivyo kusababisha kifo
hicho na majeruhi watatu”alisema.
Kamanda sadi alitoa wito kwa madereva kufuata sheria ya usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika.
No comments :
Post a Comment