……………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
Mbunge wa jimbo la
Bagamoyo mkoani Pwani Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, amegawa ndoo za
maji kwaajili ya kunawa mikono, pamoja na sabuni katika maeneo
mbalimbali ya kata ya Dunda, Nianjema na Magomeni ikiwa ni muendelezo wa
mapambano dhidi ya maamukizi ya ugonjwa wa Corona.
Ziara hiyo iliyopitia
vijiwe mbalimbali vya pikipiki na maeneo ya masoko, Dkt. Kawambwa
aliwatahadharisha wafanyabiashara na watu wanaokuja katika maeneo hayo
kupata mahitaji mbalimbali kuwa ugonjwa wa Corona ni hatari kwani
unaenea kwa kasi hivyo hakuna budi kuchukua tahadhari na maradhi hayo.
Aidha, Dkt. Kawambwa
aliwataka waendesha pikipiki kuhakikisha abiria zao wananawa vizuri
mikono yao kwa kutumia maji tiririka na sabuni hizo kabla ya kupanda
kwenye usafiri huo, kwani kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa
watajiepusha na maambukizi hayo.
“Vijana wangu
waendesha pikipiki na wafanyabiahara hakikisheni mnachukua tahadhari kwa
kiasi kikubwa kuhusu ugonjwa huu ili uweze kujikinga wewe binafsi na
familia nyumbani” alisema Dkt. Kawambwa.
“Tunaona namna
ambavyo maambukizi hayo yanavyoendelea siku hadi siku kwa nini nawe
usiunge mkono juhudi za muheshimiwa Rais Dkt. Maghufuli na viongozi
mbalimbali za kuhakikisha tunabaki salama”? alihoji.
Alisema ameongea na
wahisani waliowahi pia kusaidia katika operesheni ya macho bure ambao ni
Bilal eye camp, nao kwa kuona umuhimu wa tahadhari ambapo wamekubali
kutoa ndoo za maji na sabuni ili zitumike kunawa mikono.
Kwa upande wao
madiwani wa viti maalum, Shumina Rashidi na Afsa Kilingo waliwataka
wafanyabiashara hao wa kata hizo kushirikiana na serikali katika
kuhakikisha wanashinda vita dhidi ya corona.
Aidha, madiwani wa
kata ya Nianjema Abdul Pyallah na Diwani wa kata Dunda Dickson Makamba
walimshukuru na kumpongeza Mbunge Dkt. Kawambwa, kwa kufanikisha zoezi
hilo muhimu.
Kwa upande wao
waliopokea misaada hiyo ya ndoo za maji na sabuni kwaajili ya kunawa
mikoni wamemshukuru Mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwajili wananchi
wake hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu
unaosababishwa na virusi vya Corona.
No comments :
Post a Comment