Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amesema atachukua hatua
kwa Taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama
kubwa.
Bashungwa
alitoa onyo kwa NGOs zilizoomba kibali cha kuzalisha barakoa kwa ajili
ya kuwasaidia Watanzania lakini badala yake wanauza barakoa kwa
shillingi 2,500 hadi 3,000
“Wamekuwa wakitoa masharti kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawauzi barakoa chini ya bei hiyo”.
Sitawataja
kwa leo lakini nikiona tu wanauza kwa bei kubwa sitasita kuwachukulia
hatua, maana mnakuja kuomba vibali kumbe mnafanya mtaji.
Aliongeza
kusisitiza barakoa zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1500 badala ya bei ya
sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa changamoto
ya kumudu.
Kwa
upande mwingine Mhe. Bashungwa alivipongeza Viwanda nguo vya A-Z na
Sunflug kwa kuzalisha barakoa ambazo zinawasaidia watanzania walio
wengi, na amewahaidi serikali kuwapati ushirikiano.
Aidha
alivitaka Viwanda hivyo kuendelea kuzalisha kwa wingi ili wananchi
walio wengi wa vijijini waweze kupata vifaa hivyo vya kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa wa korona.
Kwa
upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo aliwataka wananchi
wote wa mkoa huo kuchukua taadhali zinazotolewa na Wizara ya afya
wanapotembelea maeneo yenye mkusanyiko.
Pia, alisisitiza kuwa ni vema sasa wafanyabiashara hao wakatengeneza barakoa kwa bei nafuu ili kuwezesha wananchi kununua.
Wakitoa
taarifa kwa Mhe. Waziri, Bw. Emmanuel Mgoma muakilishi wa kiwanda cha
Sunflug alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 25,000 kwa siku.
Muakilishi wa A-Z Bw. Slyvester Kazi alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha barakoa 15,000 kwa siku.
No comments :
Post a Comment