Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel
Jeremia Opulukwa akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza
itakayotumika kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani hapo
wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari katika
mapambano dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya
Saza itakayotumika kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani
hapo wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari
katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya
Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
Nicodemus Mwangela akizungumza na bodaboda wa kituo cha Stendi ya
Mkwajuni Songwe ambapo amewaelekeza kukaa mbalimbali, kunawa kwa maji na
sabuni ili kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona.
*******************************
Watu wote ambao
hawachukui hatua za tahadhari za kujikinga na kuwakinga wengine dhidi
ya
maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa kutofuata maelekezo ya
wataalamu wa Afya, watatozwa faini kwakuwa wana hatarisha maisha yao na
ya wengine.
Mkuu wa Wilaya ya
Songwe Samuel Jeremia Opulukwa amebainisha hayo jana mara baada ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe kufanya ukaguzi wa utayari wa
kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona katika Wilaya
hiyo.
Opulukwa amesema,
“Sasa tunaanza kutoza faini wote wasiofuata maelekezo ya wataalamu wa
Afya kuhusiana na Corona, mfano tukipita dukani au sehemu ya biashara na
hakuna maji na sabuni, tuta toza faini na kufunga kwa mda biashara hiyo
mpaka mtu huyo azingatie maaelekezo hayo”.
Ameongeza kuwa
lengo la Wilaya hiyo ni kuhakikisha kuwa mahali pa kufanyia biashara ni
salama kwa wafanyabiashara na watumiaji wa huduma hizo huku akieleza
kuwa wanawa fuatilia wageni wote wanao toka nje ya wilaya waliopo katika
nyumba za kulala wageni na kuchukua maelezo yao kwa ajili ya tahadhari
endapo wana dalili za Ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Opulukwa
ameongeza kuwa elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wote wa Wilaya ya
Songwe hususani katika maeneo ya migodi ambapo kuna mikusanyiko ya watu
wengi pia ameielekeza kamati inayohusika kutoa elimu ifanye ufuatiliaji
wa kina endapo wananchi wanazingatia wanayo waelekeza.
Aidha amesema
mara baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kufanya ukaguzi wa
utayari wa Wilaya hiyo katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya
Corona, Kamati hiyo imebaini baadhi ya mapungufu ambayo kama wilaya
itasimamia kuyarekebisha.
Amefafanua kuwa
yote yaliyoonekana kama mapungufu yapo ndani ya uwezo wa Wilaya ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha eneo la kuwatenga washukiwa wa Corona lina
vitanda vya kutosha na kujenga kichomea taka katika Zahanati ya Saza
ambayo itatumika kutibu wagonjwa wa Corona.
Naye Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Songwe Dkt Humphrey Masoke amesema wameshaagiza vifaa kinga
na tiba vyote muhimu katika Bohari kuu ya Dawa ili kuongezea katika
vifaa vichache walivyo navyo tayari.
Dkt. Masoke
ameongeza kuwa wana endelea kutoa maelekezo na elimu kwa jamii juu ya
tahadhari ya ugonjwa wa Virusi vya Corona kwakuwa bado baadhi ya
wananchi wanaamini ugonjwa wa Corona ni wa wazungu hivyo hauwahusu.
Estin Nyangito
Mkazi wa Mkwajuni Songwe amesema wamesha pewa elimu ya kuchukua
tahadhari ya kujikinga na Virusi vya Corona na elimu hiyo wataisambaza
kwa wananchi wengine ili nao waweze kuchukua tahadhari.
Kwa upande wake
Jakson Mwampashi Mkazi wa Songwe amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuweka
utaratibu wa kutoa elimu mara kwa mara na kwa njia mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kutumia magari ya matangazo ya barabarani ili wananchi wote
waweze kupata elimu ya Corona
No comments :
Post a Comment