Wednesday, April 1, 2020

WANAWAKE HANANG’ WANUFAIKA NA MRADI WA KILIMO KUTOKA SHIRIKA LA OXFAM & UCRT


Felista Giyam mhasibu wa kikundi cha hamasa ameiomba serikali kuona uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo
Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga anasema mradi huo  utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya miongoni mwa jamii
Albert Masuja muwakilishi kutoka shirika la UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.
Baadhi ya wakinanana wanufaika wa mradi huo wakibadilishana mawazo wakiwa sahambani kukagua mazao yanaendeleaje 
Donath Fungu Meneja wa miradi ya  Oxfam kanda ya kaskazini akitoa ufafafanuzi wa mradi huo unavyoendelea kwa sasa 
 Charles Kidaguwi mmoja wa wanaume walioshiriki katika mradi huo wa wanawake na vijana kwaajili ya kujikwamua kiuchumi katika kijiji cha Mureru wilayani Hanang’  mkoa wa Manyara.

  Anna Iselu mbaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake na vijana cha Gosanga akikagua mazao katika shamba la mradi wa wanawake na baadhi ya wanaume waliojiunga katika vikundi hivyo
 
Charles Kidaguwi ambaye ni mmoja wa wanakikundi na mlizi wa shamba la mradi akifurahia jambo 
Baadhi ya wanakikundi wakitoka kukagua shamba la mradi wa mahidi waliowezeshwa na Oxfam pamoja na  Acrt amabao wanatarajia kuvuna zaidi ya magunia 100-150 kwa mujibu wa wataalam wa kilimo.
Na Vero Ignatus,Manyara.
 
Katika kuhakikisha kuwa jamii inajikwamua kiuchumi
shirika la Oxfam Tanzania kwa kushirikiana na Ujamaa community resources (UCRT wamewawezesha jumla ya wanawake 45 katika Kijiji
Mureru kata ya Balangdalalu wilayani hanang kuanzisha mradi wa kilimo cha
umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa asilimia 100 kwa wanaume zao.
 
Wakieleza manufaa ya mradi huo kwao wanawake hao kwa
nyakati tofauti wamesemakuwa mradi huo utawafanya kutokuonekana mizigo ndani ya
familia na kwa jamii kwa ujumla na kuleta mtazamo mwingine mpya na chanya
miongoni mwa jamii wilayani hapo kufuatia jamii ziishio Hanang kutokumpa nafasi
mwanamke hivyo kuendelea kuwa na uchumi tegemezi kwa miongo yote.
 
“Huu mradi kwakweli kwanza tunawashukuru
Oxfam na Ucrt kwa kutuletea mradi huu unajua huu mradi utatukwamua sana
kiuchumi na hata kusaidia baadhi ya majukum kwenye Familia”alisema Felista
Giyam ambaye ni mhasibu wa kikundi cha wanawake hao
.
 
 Ameongeza kuwa
pamoja na mradi huu kulenga wanawake ndani yake kuna wanaume ambao tumeamua
kushirikiana nao kwani sisi tunaamini 
“hapa ndani ya mradi kuna wanaume 12 kati yet una hapo tumeamua sana katika umoja.kushirikiana kwa sababu ni mwanzo” Alisema Felista
 
Mmoja ya wanakikundi mwingine Anna Iselu pia
kwa niaba ya wanawake hao na kikundi hicho cha muungano ameiomba serikali kuona
uwezekano wa kutafuta masoko kwa mazao ya wakulima kwani wamekuwa wakilima kwa
muda mrefu lakini wanakosa masoko hivyo kuwakatisha tamaa licha ya kukiri kuwa
wamekuwa na faida kwa wastani japo soko linaendelea kuwa kikwazo licha ya
kwamba pia wakulima wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika pembejeo za kilimo.
 
 “Unajua
hapa tunatumia gharama kubwa wakati wa kununua pembejeo lakini tunakosa masoko
jambo hili linaturudisha nyuma kwakweli serikali iangalie namna ya kuwawezesha
wakulima hasa sisi wanawake ambao tumeamua kujiingiza katika kilimo

Alisema Anna Iselu mmoja ya wanakikundi.
 
Charles Kidaguwi ni
kati ya wanaume ambao wameshiriki katika mradi huo amesema kwake una manufaa
makubwa kwani utamsaidia kuwajibika vyema katika familia zaidi tofauti na awali
kwani kwake  ni  chanzo kimojawapo cha mapatao ,pia kwa upande
wa mwanamke itamsaidia kujikwamua kiuchumi,na kutoa mchango katika familia
tofauti na awali walikuwa wanakaa nyumbani pekee.
 
Kwasababu sikuzote familia inalaliaga
upande wangu lakini kama mama amepata mradi huu wa kilimo basi na mimi nitapata
msaada mkubwa alisema Chalrles Kidaguwi kutoka Kijiji cha Mureru wilaya ya
Hanang’ mkoa wa Manyara
 
Kwa upande wake Donath Fungu Meneja wa miradi
ya  Oxfam kanda ya kaskazini amesema
mradi huo wanaufanya kwa kuwashirikisha wanawake na vijana lengo likiwa ni kuwajengea
wanawake uwezo kiuchumi kipato kiuchumi kwani
mwanamke anajishughulisha na mambo mengi ila jamii haimtambui
 
Ukimuwezesha mwanamke umeiwezesha familia
,jamii na Taifa kwa ujumla hivyo Oxfam Tanzania nzima mdau wetu mkubwa
tunaesgughulika nae ni mwananmke,kitendo chake cha kutambulika  kinatokana na nguvu yake ya kiuchumi kuwa
ndogo tunaamini kwamba atakapopata nafasi ya kuinuka kiuchumi
 
Fungu amesema mwanamke atakapopata nguvu ya kuinuka
kiuchumi atapata nafasi ya kufanya maamuzi katika ngazi ya kifamilia Kijiji
hadi ngazi ya kitaifa,amesema pamoja na hayo pia wanawapatia mafunzo ya uongozi
,kujiamini ambapo hadi sasa wamefikia hatua kubwa 



Amesema hapo awali katika
wilaya hiyo mwanamke alikuwa haruhusiwi kusimamam mbele ya jamii na kuzungumza
chochote ila baada ya mafunzo waliyowapatia wameweza kujiamini na  baadhi yao wameweza kugombea nafasi
mbalimbali katika ngazi za vijiji,kuwepokatika na kamati za vijiji na nafasi
mbalimbali muhimu.
 
Naye Mratibu wa Mradi kutoka  UCRT Masuja alisema kuwa malengo ni kumpa mwanamke
fursa ili aweze kuboresha Maisha yake kiuchumi ambapo wameweza kuwaweka katika
vikundi ili waweze kufanya kazi kwa pamoja na kuleta ufanisi Zaidi
 
Amesema katika kushirikiana na Oxfam wameweza kutoa
nafasi kwa mwanamke kumiliki ardhi wapatao 365 pamoja na kuwapatia hati miliki,pia
wameweza kuwapatia wakinamama wa kikundi cha hamasa ng’ombe wapatao 9 na sasa
wamepo 18 lengo ni kuwakwamua kiuchumi pamoja na vijana kujitambua na kujiandaa
kuja kuwa na familia baada
e.
 
 
 
 

No comments :

Post a Comment