Marekani imerekodi vifo vingi vya ugonjwa wa corona kwa siku huku watu 1,736 wakifariki siku ya Jumanne.
Marekani ina wagonjwa 398,000 wa virusi hivyo waliothibitishwa , ikiwa ndio idadi kubwa zaidi duniani .
Wakati
hayo yakijiri, Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika
la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani
kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Trump
amelilaumu shirika hilo kwa kuegemea zaidi upande wa China. Rais huyo
wa Marekani amedai kwamba asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China
katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi
vya corona.
Akitoa taarifa juu ya hali ya maambukizi hayo nchini Marekani, Trump
alipuuza umuhimu wa taarifa ya mshauri mwandamizi iliyotolewa mapema
mwaka huu kutahadharisha juu ya uwezekano wa kulipuka kwa maambukizi
hayo. Rais huyo amedai kwamba hakuiona taarifa hiyo.
Badala yake Rais huyo wa Marekani amelishukia shirika la afya duniani
WHO na kulitishia kulikatia fedha.Trump amesema asasi hiyo inaegemea
sana upande wa China kuhusu mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya
virusi vya corona.
Amedai
kwamba Shirika la WHO lilishirikiana na China katika juhudi za nchi
hiyo za kupunguza hatari ya mlipuko wa maambukizi hayo.
Rais Trump amesema Shirika hilo limeisifu China ingawa pana sababu ya
kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi iliyotolewa na serikali ya China juu
ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya corona.
No comments :
Post a Comment