Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, amesema kuwa
wanamshikilia Wakili wa kujitegemea Albert Msando, baada ya kutoa kauli
za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa madai ya
kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya ili hali yeye hana mamlaka
hayo.
Kamanda
Moita ameyabainisha hayo leo Aprili 30, 2020, na kusema kuwa Msando
alikuwa anaelezea hali mbaya ya ugonjwa wa Corona ndani ya Mkoa wa
Arusha kupitia video yake iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao mbalimbali
ya kijamii, huku akiwataka waandishi wa habari wawe mstari wa mbele
katika kutoa taarifa za ugonjwa huo.
"Hali hii ilitoa wakati mgumu kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza, kauli
hii aliitoa wakati anatoa vifaa vya kujikinga na Corona katika eneo la
kaloleni katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha,
na Serikali ilikwishatoa maelekezo kuwa mwenye mamlaka ya kutoa tarifa
hizo ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu, hii kauli lazima
iheshimiwe" amesema Kamanda Moita.
No comments :
Post a Comment