Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba,
Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga (wa pili kutoka kulia) akisisitiza
namna bora ya kutumia adhabu mbadala badala ya vifungo magerezani kwa
baadhi ya makosa ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa
mahabusu/wafungwa magerezani wakati huu wa kipindi cha ugonjwa wa
Corona kwa Wahe. Mahakimu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Bukoba , Mhe. Lucia Kairo (katikati)akisisitiza jambo leo kuhusu
ufunguaji wa mashauri kwa njia ya mtandao kwa wadau wa Mahakama ili
kupunguza msongamano katika maeneo ya Mahakama na magerezani kwa upande
wa mahabusu na wafungwa ili kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona .
Baadhi ya
Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na wadau wa Mahakama
wakimsikiliza , Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Bukoba, Mhe.Lucia Kairo (hayupo pichani) katika kikao maalumu na wadau
wa Mahakama kuangalia namna bora ya kupunguza msongamano katika maeneo
ya Mahakama, yakiwemo maeneo ya magerezani kwa upande wa mahabusu na
wafungwa.
(Picha na Ahmed Mbilinyi – Mahakama Kuu Kanda, Bukoba)
No comments :
Post a Comment