Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary
Mgumba (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 30 Aprili 2020 wakati
akizungumza na viongozi wa TADCOs Co ltd kuhusu hatua iliyofikiwa ya
uagizaji wa mbolea katika ukumbi wa KILIMO IV Jijini Dodoma.
****************************
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imesisitiza kuwa
haitopanga wala kuingilia bei za mazao ya wakulima nchini badala
yake
wakulima watajipangia bei na kuuza wenyewe ilihali serikali ikisalia
kama msimamizi.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary
Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 30 Aprili 2020 wakati akizungumza
na viongozi wa TADCOs Co ltd kuhusu hatua iliyofikiwa ya uagizaji wa
mbolea katika ukumbi wa KILIMO IV Jijini Dodoma.
Mhe Mgumba amesema kuwa mfumo wa
biashara ulivyo unategemea zaidi ujazo wa mazao sokoni, hivyo bei
haitolewi kutokana na gharama alizotumia mkulima wakati wa uzalishaji
badala yake bei inaendana na soko.
Amesema kuwa wakulima kama
wanavyoruhusiwa kuzalisha kadhalika wakulima hao watauza mazao yao
popote watakapotaka wao lakini kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.
Kuhusu Mfumo wa stakabadhi ghalani
Naibu Waziri Mhe Mgumba amesema kuwa mfumo huo ulianzishwa kwa lengo la
kumrahisishia huduma za biashara mkulima hivyo utaendelea kutumika kwa
mujibu wa matakwa ya kuanzishwa kwake.
Amesema kuwa zipo changamoto
nyingi katika utekelezaji wa mfumo huo unaochagizwa na viongozi
wanaosimamia hususani wa vyama vya Ushirika kutotekeleza kwa mujibu wa
sheria.
“Mtu akipeleka mazao yake ghalani
lengo la serikali kwa sababu mazao yote tunategemea msimu wa mvua na
upatikanaji wake ni wa wakati mmoja hivyo kuhifadhi kwa pamoja na kupewa
stakabadhi itakayomrahisishia kupata mkopo kwa ajili ya kukidhi
mahitaji yake wakati akisubiri gharama za mazao zikipanda aweze kuuza
kwa bei nzuri” Alikaririwa Mhe Mgumba
Mhe Mgumba ameongeza kuwa mfumo
huo ni mzuri endapo utaendelea kusimamiwa vizuri ikiwa ni pamoja na
kuendelea kuuboresha zaidi ili uwanufaishe wakulima kote nchini kwani
mfumo huo unapunguza gharama za uendeshaji.
Ameeleza kuwa miongoni mwa
changamoto waliyokuwa nayo wakulima ilikuwa ni Tija ndogo katika mavuno
yao yaliyosababishwa na matumizi madogo ya mbolea hivyo serikali ilitoa
elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea hivyo
katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano tija imeongezeka.
Mgumba amesema kuwa matumizi
sahihi ya mbolea yameongeza tija katika sekta ya kilimo kwani uzalishaji
umeongezeka na wakulima wamekuwa na kipato kikubwa.
Katika kikao kazi hicho Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba amesema kuwa nchi ina mbolea ya
kutosha ambapo ina akiba ya zaidi ya Tani 203,000 iliyotokana na
uagizaji wa mbolea uliofanywa kwa mwaka mzima wa kiasi cha mbolea Tani
633,197
No comments :
Post a Comment