Meneja wa
kampuni ya Mega Beverages Christopher Ndossi akiwa na kamanda wa
Magereza Mkoa wa Arusha sanjari Mkuu wa mkoa wa Arusha Mara baada ya
makabidhiano hayo ya Ndoo 50 na lita 2500 ya vikatasa mikono Leo jijini
Arusha.
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea lita 2500 za vitakasa mikono na
ndoo 50 za kuoshea mikono Sanjari na hundi za fedha ikiwa ni sehemu ya
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19.
Kwa
muktadha huo ameendelea kuwataka wananchi kuendelea kuchukuwa hatua za
kudhibiti Ugonjwa wa Covid 19 kwa kufuta maelekezo na kuacha
misongamano isiyo ya lazima.
Akiongea
wakati wa Makabidhiano hayo kutoka kampuni za Mega Beverages Hanspaul
na Simba Truck Gambo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea
kuchukuwa hatua zaidi za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo
zinazoelekezwa na Serikali
Alisema
kuwa kila mmoja wetu tuache kukusanyika kwenye maeneo yenye misongamano
isiyo ya lazima na kuwataka wenye mabasi daladala kuacha kujaza na
kuendelea kuchukuwa hatua kwa kuweka maji tiririka vituoni.
“Kama
Serikali tunawashukuru Sana wadau hawa ambao wameonyesha kushirikiana
nasi katika kukabiliana na janga hili la Ugonjwa wa Covid 19 nasi
tutaendelea kuchukua hatua zaidi za kukabiliana na ugonjwa huu”
Alisema
kuwa wananchi tusijiamini Sana kwa kuwa Ugonjwa huo unaua kwa kuepuka
misongamano isiyo ya lazima na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na
Serikali huku akibainisha kuwa wanahitaji kiasi cha milioni 196 za
ukarabati wa eneo la wagonjwa kama walivyoelekezwa na Waziri wa Afya na
shirika la Afya Ila la awali limekamilika.
Awali
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alisema kuwa tangia
tukio la kwanza kutangazwa wamekuwa wakishirikiana na wadau jinsi ya
kupata vifaa sanjari na utoaji wa elimu ikiwemo ushiriki wa juu ya
mapambano ya Covid 19.
Alisema
kuwa kumekuwa na mahitaji mengi ya vifaa ndani ya jamii yetu na kama
Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuona jinsi ya
kusaidiana kupata vifaa kuisaidia jamii.
Kwa
Upande wao Meneja wa Mega Beverages Christopher Ndossi na Mkurugenzi wa
Hanspoul na Mkurugenzi wa Simba Truck wamesema kuwa wataendelea
kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaendeleza kupambana
Ugonjwa huo na huo ni mwanzo wa msaada huo.
|
No comments :
Post a Comment