**********************************
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe
Emmanuel Shilatu akiambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Tarafa
wameongoza msako mkali wa kukagua utekelezaji wa bei elekezi ya sukari
iliyotolewa na Serikali hivi karibuni.
Gavana Shilatu
alipita kwenye maduka ya jumla na ya rejareja kuona namna
Wafanyabiashara wanavyouza sukari ambapo kwa bei ya rejareja hawatakiwi
kuuza zaidi ya bei ya Tsh. Elfu tatu (3,000/=) kwa kilogram moja na
kukuta maduka mengi wametii agizo la Serikali na kuwasihi Wananchi kutoa
taarifa mara moja kwa Serikali ya Kijiji au ya kata endapo watabaini
ukiukwaji wa bei elekezi ya Serikali.
“Nimepita kwenye
maduka na nimejionea utiifu wa Wafanyabiashara wanavyouza sukari.
Niwasihi Watendaji kata na vijiji waendeleze msako kwenye maeneo yao na
kuwafichua wanaouza Sukari kwa bei ya kulangua. Ni jukumu letu sote
kuwatetea Wananchi wetu wasiuziwe sukari kwa bei ya ulanguzi na ole wake
Mfanyabiashara atakayekiuka maelekezo ya Serikali tutamchukulia hatua
Kali tutakapo mbaini.” Alisisitiza Gavana Shilatu.
Katika ziara hiyo
Gavana Shilatu aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Tarafa.
Serikali imeingilia kati kwa kutoa bei elekezi ya sukari kufuatia
Wafanyabiashara wasio waaminifu kutaka kuwalangua Wananchi, jamii
inaaswa kuwafichua Walanguzi wanaokiuka maagizo ya Serikali.
No comments :
Post a Comment