*****************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika
ya haki za binadamu na watu yenye makao makuu yake jijini Arusha
,imejipanga kumuenzi aliyewahi kuwa
rais na Jaji wa mahakama hiyo
marehemu Augostino Ramadhani ,aliyefariki April 28 mwaka huu.
Jaji wa mahakama hiyo Blaiset
Tchikaya ,amesema leo ofisini kwake kwamba marehemu Jaji Ramadhani
alikuwa ni kiungo muhimu katika utendaji wa kazi wa mahakama hiyo kwa
sababu alikua akijua mambo mengi hasa ya kijamii pamoja na sheria za
kimataifa.
Amesema kuwa Jaji Ramadhani alikuwa rais wa mahakama hiyo kwanzia mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 .
Amesema Mahakama hiyo katika
kumuenzi Jaji Agustino Ramadhani juu ya utendaji wake imeteua kamati ya
watu kumi na mmoja itakayojadili namna bora ya kutoa tuzo maalumu ya
kumuenzi .
Kwa upande wake Faraji Mtolela,
ambaye amewahi kufanya kazi pamoja Na marehemu Jaji Agustino Ramadhani
ameseama jaji huyo alikuwa mkarimu, zaidi ya jaji ni sawa na baba kwao
na pia alipenda watu wafuate maelekezo pamoja na taratibu zote za
mahakama ya Afrika.
Naye mwandishi wa gazeti la the
citizen Zephania Ubwani amesema kuwa Jaji Ramadhani ezi za uhai wake
aliweza kutoa mchango mkubwa katika haki pamoja na utekelezaji wa
sheria za haki za binadamu, pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa kwa
waandishi wa Habari.
Alisema kuwa Jaji Ramadhani wakati
akiwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu alikuwa
mstari wa mbele kuona mahakama hiyo inakuwa na kujenga misingi ya
kuheshimu utu na haki za binadamu.
ReplyReply allForward |
No comments :
Post a Comment