Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea wakati akifungua mafunzo ya jinsi ya kuepuka maambukizi ya
Virusi vya Corona kwa viongozi wa dini mbalimbali waliojitokeza katika
Ukumbi wa Karimjee jijini Dar Es Salaam.
Mwakilishi mkazi wa Shirika la
Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Katisela akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo kwa viongozi wa dini kuhusiana na jinsi ya kuepuka maambukizi
ya ugonjwa wa Corona usiingie nchini.
Mwakilishi mkazi wa Shirika la
Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Katisela akizungumza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo kwa viongozi wa dini kuhusiana na jinsi ya kuepuka maambukizi
ya ugonjwa wa Corona usiingie nchini.
Baadhi ya viongozi wa dini
waliofika katika mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na maambukizi ya
ugonjwa wa Corona unaoendelea kusambaa duniani. Mafunzo hayo
yameandaliwa na Wizara ya Afya na kushirikisha viongozi wa dini
mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja ya Waziri Ummy
Mwalimu akiwa na viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa maendeleo
waliofika katika mafunzo ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa
wa Corona yanayofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar Es Salaam.
………………………………….
Waziri Ummy Mwalimu ametoa masaa 5
kwa kila Halmashauri kutenga...
sehemu maalum kwaajili ya kumuweka
mshukiwa wa ugonjwa wa Corona na kufanya utaratibu wa uchunguzi na kutoa
taarifa haraka Wizara ya Afya.
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo
wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa dini nchini jinsi ya kuepuka
maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinazidi kusambaa katika nchi
mbalimbali duniani. “Ninatoa muda mpaka saa 10 jioni vituo vyote vya
afya vya umma nchini viwe vimetenga sehemu maalum ya kuweka mshukiwa wa
Virusi vya Corona na kuripoti haraka iwezekanavyo katika Wizara ya Afya
kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki”. Amesema Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy amesema mpaka sasa
nchi yetu ni salama, hakuna mshukiwa wa COVID19 lakini Serikali imeweka
mikakati mbalimbali ya kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini ikiwa ni
pamoja na kushirikisha taasisi mbalimbali za dini. “Tunawaomba viongozi
wa dini muende mkatoe elimu kwa waumini wenu kuchukua tahadhari kwa
kuzingatia kanuni za usafi na pia kukaa mbali na mtu mwenye dalili za
mafua ambaye ana historia ya kusafiri nje ya nchi”. Mhe. Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ametoa
maelekezo kwa taasisi za dini, taasisi za umma, maofisi na mashule ya
Serikali na binafsi kuweka sehemu maalum ya kunawa mikono kwa maji yenye
dawa ya kuua bakteria (hand sanitizers) ili kuepuka maambukizi
yatokanayo na bakteria
No comments :
Post a Comment