*******************************
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali itawachukulia hatua watu wote
waliohusika na ubadhilifu wa mali zikiwemo nyumba za Mamlaka ya Mkonge
Tanzania.
Pia, Waziri Mkuu
amesema Serikali itafanya uchunguzi katika mashamba yote ya mkonge ili
kubaini yameendelezwa kwa kiasi gani na sehemu ambazo hazijaendelezwa
zitachukuliwa na kugawiwa kwa wananchi ili walime mkonge.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo(Jumanne, Machi 3, 2020) wakati akizungumza kwa
nyakati tofauti na wananchi wa kata za Segera na Kabuku akiwa katika
ziara yake ya kikazi wilaya ya Handeni, Tanga.
Machi 1, mwaka
huu Waziri Mkuu alipokea taarifa ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali
katika tasnia ya kilimo cha mkonge mkoani Tangana kuagiza mapendekezo
yaliyotolewa na timu hiyo yakiwemo ya kurejeshwa Serikalini kwa nyumba
na. 176 eneo la Bombo ambayo ilimilikishwa kwa Bw. Salum Shamte
yafanyiwe kazi.
Nyumba
nyingine zilizopendekezwa kurejeshwa Serikalini ni pamoja na nyumba kumi
zilizoko ndani ya Jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone, Bombo,
Nguvumali na Market street ambazo zilinunuliwa na watumishi hao kwa
udanganyifu.
Timu hiyo
maalum ya uchunguzi iliundwa na Waziri Mkuu na ilifanya uchunguzi mkoani
Tanga kuanzia tarehe 29/11/2019 hadi tarehe 07/02/2020. Timu hiyo
iliyokuwa na wajumbe 13 ilihusisha maafisa kutoka ofisi mbalimbali za
Serikali.
Waziri Mkuu
amesema kwa kuwa katani ndio zao la biashara mkoani Tanga Serikali
itahakisha watu wote wenye mashamba makubwa ya mkonge ambayo wameshindwa
kuyaendeleza itayachukua na kuyarejesha kwa wananchi.
Wakati huo
huo,Waziri Mkuu amesema Serikali imejenga vituo 352 vya afya nchi nzima
vikiwemo viwili vilivyojengwa Handeni, kutokana na mahitaji makubwa ya
huduma hiyo kata ya Segera itapewa kipaumbele katika awamu ya pili ya
ujenzi.
Kadhalika, Waziri
Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ahakikishe
wananchi wanaokwenda kufuata huduma za matibabu katika vituo vya afya na
zahanati wanapatiwa dawa badala ya kuelekezwa kwenda kununua kwenye
maduka ya watu binafsi.
Alisema Serikali
imeongeza bajeti ya dawa kutoka sh. bilioni 37 hadi sh bilioni 269,
hivyo hakuna sababu ya mwananchi kwenda kwenda eneo la kutolea huduma ya
afya na kukosa dawa.
Pia, Waziri Mkuu
alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Handeni ahakikishe kila kijiji kinapata
huduma ya maji safi na salama kwa kusimamia uchimbaji wa visima kupitia
fedha za makusanyo ya ndani.
Waziri Mkuu
amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua
mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini
wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.
Kuhusu suala la
umeme, Waziri Mkuu amesemamaeneo ya wilaya hiyo ambayo bado hayajapata
umeme yote yatasambaziwa umeme kupitia Mradi wa Nishati Vijijini (REA)
na wananchi hawatowajibika kulipia gharama za nguzo.
Amesema Rais
Dkt. Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inawaka umeme tena
kwa gharama nafuu ya sh. 27,000, hivyo amewataka waendelee kuwa na imani
na Serikali yao.
No comments :
Post a Comment