Naibu waziri wa Mifugo akisafisha Mikono yake kwa maji yanayotiririka katika mnada wa Miserani.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
Akiwa na mbunge wa Monduli Julius Kalanga,wa Pili Kulia Pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri huyo Isaack Joseph wakati alipotembelea mnada
wa Miserani uliopo wilayani Monduli.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi akiwa ndani ya Boda wakati alipotembelea kituo Cha Mifugo na Uvuvi.
**********************************
Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wafugaji nchini
kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari juu ya virusi vya homa ya Mafamu
Covid -19 ambavyo vinasababisha Ugonjwa wa Corona.
Akizungumza
na wafugaji mara baada ya kutembelea minada ya mifugo katika soko la
kimataifa la mifugo lilipo wilayani longido pamoja na mnada wa
Miserani,uliopo wilayani monduli mkoani Arusha,Ulega alisema kuwa
tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa wafugaji na
wafanyabishara wanawana mikono.
Aidha alisema
kuwa pindi biashara ya mifugo inapofanyika ili kuepuka mikusanyiko
isiyo ya lazima ni vyema wafugaji wakarejea majumbani ili kujikinga na
gonjwa hilo.
Katika hatua
nyingine naibu waziri Ulega alitembelea kituo cha wizara ya mifugo na
uvuvi kilichopo katika boda ya namanga na kuzungumza na maafisa
hao,ambapo alisema kuwa serikali imeruhusu biashara kufanuyika kama
kawaida hivyo waisaidie serikali katika eneo hilo.
Alisema ni
lazima biashara na shughuli za kiuchumi ziendelee ili serikali ipate
mapato, huku familia zipate mahitaji yao muhimu.
“Hatuwezi
kufunga minada hii sababu maisha ya watanzania walio wengi huishi kwa
kutafuta mlo a kila siku, hivyo kuzuia minada hii ni sawa na kuataka
wafe kwa njaa, sasa hili serikali tumelitafakari ka kina na tumeona
haifai kuifunga minada hii,”alisema.
“Ninachosisitiza
hapa kwenye minada hii wawepo tu wale wanaouza mifugo na wanaonunua,
lakini mkishauziana tu ondokeni mara moja mnadani na sitaki muweke
mikusanyiko,”alisema.
Aidha alipongeza minada hiyo kutokana na tahadhari zilizochukiwa
ambapo ili kuthubiti mikusanyiko makundi ya wafugaji na wafanyabishara
imepungua kwa kiasi kikubwa tangu kulipozuka Ugonjwa huo huku kila
anayeingia ananawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.
Mkuu wa
Wilaya ya Longido, Frack Mwaisumbe,alishukuru serikali kuruhusu
wananchi wake kuendelea na minada ya mifugo, sababu ni sehemu ya maisha
yao,huku akieleza wazi kuwa hapo awali minada huo wa longido ulifunngwa
kutokana na kuzua taaruki kubwa kwa wananchi mara baada mgonjwa wa
kwanza wa Corona kutangazwa.
No comments :
Post a Comment