Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela (aliyevaa miwani) akikagua orodha
ya bidhaa ambazo zimetolewa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kutokana na kuwa
zimekamatwa kwa njia za njia za magendo na wamiliki hawakujitokeza.
Simenti iliyokamatwa kwa kuingizwa
nchini kwa njia za Magendo katika Mpaka wa Tunduma ikitolewa kwa ajili
ya kupelekwa katika shule za sekondari za Mkoa wa Songwe.
……………………………………………………………………………………………………..
Mamlaka ya Mapato
Nchini (TRA) Mkoa wa Songwe imegawa baadhi ya bidhaa zilizo
kamatwa kwa
kuingizwa Nchini kupitia mpaka wa Tunduma kwa njia za Magendo ili
kukwepa ushuru.
Akipokea bidhaa
hizo kutoka Kwa Kaimu Meneja TRA Mkoa wa Songwe, Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amesema bidhaa hizo zinapelekwa katika
shule za Sekondari za Mkoa wa Songwe ili ziweze kuwasaidia wanafunzi.
“Nimepokea
simenti mifuko 192, mafuta ya kupikia ndoo 37 na sukari katoni 70
ambavyo vyote navielekeza katika shule za Sekondari ili vikasaidie
huko.” , amesema Brig. Jen. Mwangela.
Amesema mifuko
100 ya simenti ameelekza ipelekwe Wilaya ya Momba ambapo kuna ujenzi wa
shule ya sekondari ya Wasichana kwa kidato cha tano na sita na sukari
imetolewa kipaumbele Wilaya ya Mbozi ambayo watakuwa wenyeji wa
wanafunzi wa Michezo ya Umiseta.
Brig. Jen.
Mwangela amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia bidhaa hizo
ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Momba Juma Said Irando ametoa wito kwa wananchi na
wafanyabiashara waliozoea kutumia njia zisizo halali kuingiza bidhaa
nchini Kupitia Mpaka wa Tunduma waache maramoja kwani kamati ya Usalama
ya Wilaya yake imeimarisha doria ili kumaliza tatizo la wakwepa kodi.
Irando amewata
wafanyabiashara kutumia njia halali pia wazingatie sheria na taratibu za
forodha ili waweze kufanya bishara halali na kuepuka hasara kwakuwa
watakamatwa.
Amesema kuwa
wafanyabiashara watambue kuwa wakikamatwa na bidhaa ambazo zimeingizwa
Nchini isivyo halali sio tu watataifishwa mali hizo bali sheria
zinawataka walipe kodi na faini ili wachangie pato la Nchi.
Irando ameongeza
kuwa Wilaya yake imepokea mifuko 100 ya simenti ambayo itasaidia katika
ujenzi wa Sekondari ya Wasichana ambayo itakuwa sekondari ya A level kwa wasichaa pekee Mkoa wa Songwe.
Kwa upande wake
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Songwe Farensi Mniko amesema walifanikiwa
kukamata bidhaa hizo kutokana na kuimarisha kaguzi mbalimbali katika
Mpaka wa Tunduma pia kwa kupata taarifa kutoka kwa wananchi mbalimbali.
Mniko ameongeza
kuwa bidhaa zilizo kamatwa zikikaa muda mrefu bila mhusika kuzichukua
Kamishna wa TRA anayo mamlaka ya kuzigawa kwa taasisi za serikali kama
alivyo fanya kwa bidhaa za simenti, sukari na mafuta alizozitoa.
Ameongeza kuwa
bidhaa hizo hukaguliwa ubora wake kabla hazijagawiwa kwa taasisi za
serikali hivyo zinakuwa salama, huku akiwasisitiza wafanyabiashara
waache kupita njia zisizo halali kwakuwa TRA imejipanga kukomesha
magendo.
No comments :
Post a Comment