Wednesday, March 4, 2020

Tanzania Kuuza Makontena 200 ya Maharage nchini Ubelgiji 0


 
Maharage aina ya haricots vertz(green thin beans) yaliyopata soko nchini Ubelgiji.
Balaozi Jestas Abuok Nyamanga akiwa amebeba maharage yaliyopata soko la kununuliwa na kampuni
ya
  CBG-Charlier-Brabo Group ya nchini Ubelgiji.
Kulia kwake ni Wim Vandenbus scheambayeni Meneja Mauzo na Ununuzi wa kampuni, na kushoto kwa Balozi Nyamanga ni Bi Martine Danneel, ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni. Kushoto zaidi kwa Balazo ni Dr. Geoffrey B. Kabakaki, Afisa Mkuu wa Ubalozi kwa
masuala ya uchumi na biashara.
Balozi akiangalia bidhaa aina ya nanasi zilizokatwa na kuifadhiwa katika kopo na kampuni hiyo ambazo pia zinaweza kuagizwa kutoka Tanzania

Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji umepata soko kubwa la
maharage machanga ya kijani yanayojulikana kama haricots vertz(green thin beans) nchini Ubelgiji.
Soko hilo limepatikana baada ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kufanya mazungumzo
na uongozi wa juu wa kampuni ya
CBG-Charlier-Brabo Group inayonunua maharage hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuyauza katika supermarkets kubwa za Carrefour, Delhaize na Aldi za nchini Ubelgiji, Luxembourg na nchi nyingine za Ulaya.
 
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 3 Machi 2020, kampuni hiyo ipo tayari kununua containers kati ya 180-200 za maharage hayo kila mwaka kutoka Tanzania. 
 
Kupatikana kwa soko la maharage hayo nchini Ubelgiji ni habari njema kwa wakulima wa
Tanzania na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo hususan wa aina hiyo ya maharage
ambayo tayari Tanzania inayauza nchini Uholanzi.
 
Kampuni hiyo pia imeonesha utayari wa kununua aina nyingine ya maharage ijulikanayo kama
red kidney beans na chickpea kwa kiwango cha containers 8 kila mwaka katika hatua za mwanzo.
 
Ubalozi wa Tanzania unatoa wito kwa Watanzania kuchangamkia upatikanaji wa soko hilo jipya
nchini Ubelgiji kwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ya www.cbg.be au kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki kwa maelekezo zaidi.

No comments :

Post a Comment