……………………………………………………………………………………………………..
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
ametimiza ahadi yake kwa kuwakabidhi Mama lishe wa Stendi kuu ya mabasi
Mbeya jiji vitendea kazi maalum vya kutumia wakati wa
kuhudumia wateja
wao (Aprons) ambapo jumla ya vitendea kazi vimetolewa, pamoja na hilo
Dkt. Tulia ametimiza pia ahadi ya kutoa TV ambayo itakuwa inawawezesha
abiria wa kituo hicho kufuatilia matukio mbalimbali pamoja na habari
wakati wakisubiri kusafiri.
“Siku ya leo hatujaja kutekeleza
kila ahadi kwasababu hapa tuna machinga ambao nao pia wanasubiri baadhi
ya ahadi tulizozitoa lakini wakati tukiendela kuvuta subira hizo
tumekuja kuwakabidhi mama lishe Aprons 200 kwa ajili ya kulinda nguo zao
pamoja na kukaa katika hali ya usafi”
“Lakini pia tulipokuja kukabidhi
jezi kwa ajili ya maafisa usafirishaji tulisomewa changamoto nyingine
ikiwemo watu kupata taarifa mbalimbali kwahiyo siku ya leo tumeweza
kuleta pia TV ukizingatia kwasasa tunaye kijana wetu Mbwana Samatta
akikipiga kule Aston Villa naye tutakuwa tunaweza kumtazama lakini pia
na taarifa nyingine za habari zikiwemo zinazomuhusu Rais wetu mpendwa
Magufuli na Serikali yake”-Dkt. Tulia Ackson Cc @tulia.ackson
No comments :
Post a Comment