………………………………………………………………………………………….
NA FARIDA SAIDY MOROGORO
Mvua zinazoendelea kunyesha
katika maeneo Mbalimbali Mkoani Morogoro zimesababisha Vifo vya watu
wawili jana March 6 majira ya saa moja usiku katika Mtaa wa
Kihimbwa
Kata ya Boma Manispaa ya Morogoro.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bw
Antopas Ally amezungumza hayo na waandishi wa habari mara baada ya
kufika Eneo husika na kusema kuwa waliokumbwa na maafa hayo ni mwanaume
na mwanamke ambao walikuwa wanapata vinywaji katika duka moja lililopo
karibu na daraja mtaani hapo.
Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi
wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dk Ritha Liamua amekiri
kupokea miili ya watu wawili hosptitalini hapo,huku akisema kuwa hakuna
majeruhi waliowapokea mpaka sasa.
No comments :
Post a Comment