
……………………………………………………………………………
Na Bashiri Salum,Morogoro.
Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA
wametakiwa kuanzisha maduka ya mbegu katika maeneo
walipo wakulima ili
kuwapunguzia gharama ya kuzifuta Morogoro mjini.
Akizungumza na watumishi leo
alipotembelea taasisi hiyo Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema
ASA ni Taasisi pekee ya mbegu nchini hivyo inatakiwa kuwafika wakulima
wote nchini.
Huduma ya mbegu bora inatakiwa na
kilia mkulima hivyo ni lazima ASA wafikirie namna ya kushusha huduma
zao chini kwa wakulima wadogo tofauti na ilivyo kwa sasa alibainisha
Katibu Mkuu.
Akitolea mfano wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro ambako ASA wanalo shamba kubwa la kuzalisha mbegu-(Msimba seed farm) Katibu Mkuu amesema wakulima wa maeneo hayo wanalazimika kwenda Morogoro mjini kununua mbegu
“Naagiza muanzishe maduka ya mbegu
bora katika maeneo muhimu ili wakulima wapate mbegu bora zitakazosaidia
kuongeza uzalishaji wa mazao yao. Ningependa kuwepo na mahusiano mazuri
kwenye Halmashauri zinazowazunguka kwa kuweka maduka ya mbegu zenu iwe
nafuu kwa wakulima wao kutozifuata mbali”.Alisema Katibu Mkuu.
Aidha ameipongeza taasisi hiyo kwa
kuweza kuongeza uzalishaji wa mbegu bora na kutumia rasilimali zake za
mashamba kuwapatia makampuni mengine ya mbegu ili uzalishaji wa mbegu
uweze kuimarika.
Hata hivyo amewataka watumishi wa
ASA kufanya kazi kwa ushirikiano na uadilifu ili kuongeza ufanisi katika
kazi ambapo itawafanya kufikia malengo waliojiwekea.
Awali Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt.
Sophia Kashenge amesema wamejipanga kuanzisha wakala watakaosaidia
usambazaji wa mbegu nchi nzima ili wakulima wadogo waweze kufikiwa na
mbegu hizo ambazo ni bei nafuu.
Hata hivyo Dkt Sophia amesema
kiasi cha mbegu kinachozalishwa na ASA Pamoja na makampuni mengine ni
tani elfu 59 ambazo kati ya hizo tani elifu 35 ni mbegu za pamba hivyo
kiasi kilichobaki ni tani elfu 24 ambazo ni mazao mengine.
Amebainisha kwamba bado kama taifa
kuna changamoto ya mbegu na kumuomba Katibu Mkuu ziangaliwe jitihada
nyingine za kuifanya sekta ya mbegu kuwa kivutio ili sekta binafsi
ziweze kuendelea kuwekeza .
Hata hivyo watumishi wamemuomba
Katibu Mkuu kusaidia vitendea kazi vikiwemo magari na maghala katika
mashamba ya mbegu pamoja na ukarabati wa barabara za kuingia mashambani
ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mbegu bora.
No comments :
Post a Comment