Wednesday, March 4, 2020

KANZIDATA YA WATOA HUDUMA ZA KIFEDHA ITAONGEZA UFANISI KIUCHUMI, WATOA HUDUMA KUANZA KUSAJILIWA MACHI MWAKA HUU


Bw. Bernrad Dadi Mkurugenzi wa Mfumo wa Malipo wa Taifa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) aktoa mada kuhusu  Kanzidata ya Kudumu ya Watoa Huduma za Kifedha Financial Services Register (FSR) katika semina  ya waandishi wa habari  kutoka vyombo mbalimbali vya habari  inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha leo.
Bw. Augustine Hotay Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akitoa mada kuhusu matumizi safi ya Noti  na utambuzi wa alama muhimu zilizopo katika Noti.
Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akizungumza na washiriki wa semina ya Uchumi na Fedha inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki katika semina hiyo wakiangalia alama muhimu zilizopo kwenye Noti ya Shilingi elfu 10.000.
………………………………………..
Benki Kuu ya Tanzania BoT imeanzisha mfumo mpya wa huduma za kifedha  kwa
kushirikiana na wadau wengine ambao ni  CDC, TIRA TCDC CMSA na TAMISEMI ili kutengeneza Kanzitada itakayowaorodhesha  watoa huduma wote wa shughuli  za Kifedha.
Bw. Bernrad Dadi Mkurugenzi wa Mfumo wa Malipo wa Taifa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) amesema hayo mara baada ya  kutoa mada kuhusu  Kanzidata ya Kudumu ya Watoa Huduma za Kifedha Financial Services Register (FSR) katika semina  ya waandishi wa habari  kutoka vyombo mbalimbali vya habari  inayoendelea kwenye tawi la BoT jijini Arusha leo.
Amesema hapo mwanzo BoT ilikuwa ikipata taarifa  au data kwa kutumia  tafiti ambazo zilikuja kuonekana zina mapungufu kwasababu  zilikuwa zinachukua muda kupatikana   lakini pia ilikuwa ni gharama kubwa kwa sababu ili kupata hizi data au taarifa ilibidi kuajili kampuni au kikundi ili kutapita nchi nzima ili kukusanya  taarifa hizo.
Amesema Mwaka 2012 na 2014, tafiti mbili za kijiografia za maeneo ambayo huduma za kifedha
hupatikana zilifanyika Tanzania na FSDT kwa niaba ya Benki kuu ya Tanzania, ukiangalia hapo utagundua ni kipindi cha mwaka mzima ulipita  hivyo utaona hapa katikati kulikuwa na watoa huduma ambao  hawakusajiliwa.
Ameongeza kuwa jambo lingine lilikuwa ni kwamba taarifa hizi ziko maeneo mbalimbali,  Kwa mfano  ili kujua mawakala wa bima  ilibidi lazima uende TIRA kupata taarifa zao, Ili kujua  mawakala  kampuni za simu ilibidi kwenda Tigo, Vodacom, Airtel na kadhalika  na ukitaka kupata taarifa za SACCOS ilibidi  pia uende kwenye SACCOS zao , hivyo  ilikuwa vigumu sana kupata taarifa sahihi.
Bw. Bernrad Dadi amesema  hili ndilo lililofanya wasimamizi wa huduma za fedha  BoT na wadau wengine  kama CDC, TIRA TCDC CMSA na TAMISEMI kukaa pamoja na kutengeneza Kanzitada hiyo ambayo iitatupa faida Watunga sera  kujua  wapi huduma hazijafika,  Wawekezaji  kujua wapi hawapo hapa nchini ili kujipanga kupeleka huduma sehemu ambazo hawapo.  Lakini pia kuwajua watoa huduma za kifedha wakubwa na wadogo popote walipo na shughuli  wanazofanya.
“Wasimamiiaji wa huduma hizi hatuna tena sababu ya kwenda Tigo , Halotel, Vodacom na maeneo mengine  ili kujua  ana mawakala wangapi,  taarifa hizo tutakuwa tunazipata kwa pamoja na kuzitoa kwa pamoja . pia itasaidia  katika utekelezaji wa Sera za nchi ambazo tunaita (National Financial  Inclussion Framework) ambazo zinatekelezwa”. Amesema Bw. Dadi.
Ameongeza kuwa utengenezaji au uundaji wa Kanzidata yenyewe umeshakamilika kwa asilimia  98 yamebaki mambo ya taarifa  mbayo watumiaji watatuambia na kushauri namna ya kuziweka taarifa hizo.
 Usajili wa watoa huduma hao awamu ya kwanza  utaanza  mwezi huu wa Machi  na Aprili ambapo na  awamu ya pili ya usajili huo itafanyika  mwezi  Mei na Juni mwaka huu.
Ameongeza kuwa itakapofika Julai  Mosi mwaka huu mfumo huu utakuwa uko tayari na una taarifa zote , baada ya hapo wataachiwa  watoa huduma wakubwa ambao wataendelea  kuwasajili watoa huduma wapya  kadiri watakavyoandikisha, baada ya hapo tutakuwa tunawajua watoa huduma wote wakubwa na wadogo  nchini.
Amesema ukishawaunganisha watoa huduma hao na mifumo mingine kama vile Tanzania InteBank Payment  System (TIPS) utakuwa na uwezo wa kujua hela hizi zimetoka mkoa huu na kwenda mkoa huu  na  kwa  kutumia Kanzidata hii tutajua  na kupata takwimu sahihi za miamala ya fedha iliyofanyika na kuleta ufanisi wa huduma za kifedha nchini .

No comments :

Post a Comment