Wednesday, March 4, 2020

KALEMANI AONYA ULAZAJI NGUZO ZA UMEME OVYO BARABARANI


Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa mameneja pamoja na wakandarasi kuondoa nguzo za umem zilizolazwa ovyo barabarani akiwa njiani kwenda kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kuwasha umeme.
 
Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga,akizungumza kabla ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,kabla ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia,akizungumza na wananchi kabla ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,kabla ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani,akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Chemba
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewaonya wakandarasi nchi nzima wanaotelekeza miradi ya...
umeme vijijini (REA) kuacha mara moja tabia ya kulaza ovyo nguzo za umeme barabarani huku zikikaa muda mrefu bila kusimikwa.
Waziri Kalemani ametoa onyo hilo wakati akiwasha umeme katika kata ya Farkwa wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Akiwasha umeme kwenye kata hiyo, Waziri Kalemani ameshuhudia kuzagaa kwa nguzo barabarani jambo lililomkera na kuagiza wakandarasi hao kuacha tabia hiyo.
“Kuna shida moja naomba nitoe onyo la mwisho nimepita barabarani nguzo zimelala, Meneja wa Kanda na Mkoa simamia haya nimetoa siku tatu kwa nguzo zote zilizolala kwenye mkoa wote wa Dodoma ziondolewe zikajengwe tofauti na hivyo Mhandisi uache kazi na wewe mkandarasi tutakuandikia barua ya kusitisha mkataba wako,”amesisitiza.
Aidha, amemtaka Meneja wa Mkoa wa Dodoma kusimamia suala hilo na kumtaka kumwandikia barua mkandarasi atakayeshindwa atakayeacha nguzo hizo zikikaa muda mrefu na kuoza.
“Hatuwezi kuacha fedha ya serikali ikichezewa kwa kuacha nguzo ziendelee kuoza, hili ni onyo la mwisho na ni onyo kwa wakandarasi wote nchi nzima ni marufuku nguzo kulazwa chini zikifika ndani ya siku tatu zikasimikwe wananchi wapate umeme,”ameonya.
Kwa upande wake, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia amesema  umeme huo utasaidia kubadilisha maisha yao ya kila siku kwa kufanya biashara za kujiongezea kipato.
Naye, Mkuu wa wilaya ya Chemba Simon Odunga, ameishukuru serikali kwa kupeleka umeme kwenye eneo hilo na kwamba kumechangia kuongeza maendeleo katika eneo hilo. 

No comments :

Post a Comment