………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna, Dodma
Serikali ya Tanzania imesema imetenga eneo lenye Jumla ya ekari 328.6 kwa ajili ya ujenzi wa
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Felister Bura (CCM)
aliyetaka kujua ni lini uwanja wa Michezo utaanza kujengwa kutokana na
serikali kupata ufadhili kutoka Serikali ya Morocco.
Dk Mwakyembe amesema baada ya
kutenga eneo hilo serikali imefanya tathimini ya mazingira, kijamii na
kuandaa mchoro wa awali wa uwanja huo.
Dk Mwakyembe amesema Serikali mbili za Tanzania na Morocco
zinaendelea na mawasiliano kuhusu kukamilisha mradi wa ujenzi wa uwanja
wa huo.
“ Maandalizi yote ya msingi kuhusu ujenzi wa uwanja wa mpira wa
miguu tayali yamekamilika na tunaendelea kufanya mawasiliano na serikali
ya Morocco ili kuweza kukamilisha mradi huo”, ameongeza Dk Mwakyembe.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa mradi huo
unatokana na ahadi za Mfalme Mohamed VI alipofanya ziara yake Tanzania
Oktoba, mwaka 2016 alitoa ahadi ya kufadhili miradi mbalimbali nchini
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mchezo wa mpira wa
miguu.
Dk Mwakyembe amesema kuwa Serikali iliamua Uwanja huo ujengwe katika Jiji la Dodoma eneo la Nane Nane ambapo ndo makao makuu ya nchi.
Dk Mwakyembe amesema kuwa Serikali iliamua Uwanja huo ujengwe katika Jiji la Dodoma eneo la Nane Nane ambapo ndo makao makuu ya nchi.
No comments :
Post a Comment