Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti
za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akitoa mada kuhusu mapitio ya
maendeleo ya uchumi nchini, kikanda na dunia na matarajio kwa mwaka
2020.
………………………………………………
Tunapoongelea kuhusu dhana ya
ukuaji wa uchumi maana yake ni ongezeko la shughuli za
uzalishaji mali
wa bidhaa na huduma nchini.
Shughuli hizi zinapokuwa
zinaongezeka ina maana kwamba ni ongezeko kwenye kipato cha mwananchi
kwa sababu ni mwananchi mmoja mmoja na makampuni ndiyo
yanayojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti
za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango ameyasema hayo mara baada ya
kuwasilisha mada katika semina ya waandishi wa habari za uchumi na Fedha
inayoendelea katika tawi la BoT jijini Arusha
Amesema kwa miaka ya hivi
karibuni uchumi wetu umekuwa ukikua kwa asilimia 7 kwa mwaka 2018 na kwa
mwaka uliotangulia uchumi wetu ulikuwa kwa asilimia 6.8 na ukichukua
wastani wa ukuaji wa uchumi kwa miaka mitano ya nyuma iliyopita kutoka
2018 mpaka 2014 uchumi wetu ulikuwa kwa asilimia 6.7.
Akielezea zaidi Dk Misango
amesema uchumi unapokuwa unakuwa ni ongezeko la la kipato na sehemu ya
kipato hiki kinachukuliwa na serikali kwa njia ya kodi ambapo serikali
inachukua hizi fedha kwa ajili ya matumizi ya serikali.
Amesema katika Matumizi haya
fedha hizi ndizo zinazotumika katika shughuli za maendeleo kama vile
kujenga miundombinu ya Barabara, Shule, Reli , Umeme, huduma za afya
,Jamii na shughuli zingine za usimamizi wa maendeleo kwa ujumla wake.
Ameongeza kuwa kutokana na
shughuli za uzalishaji mali kuongezeka. Kazi ya BoT ni kuhakikisha
kwamba inatoa fedha kulingana na mwenendo wa ukuaji wa uchumi, na kwa
kadri uchumi unavyokua BoT inahakikisha kiasi cha fedha kilichopo kwenye
uchumi kipo kwenye kiwango kinachohitajika.
Amesema kuwepo kwa fedha mtaani
kunategemea shughuli za uzalishaji mali na shughuli za maendeleo
kuongezeka kwa sababu BoT inatoa fedha kwenda kwenye uchumi kwa njia kuu
mbili moja inatoa kwa serikali kwa ajili ya kulipia miradi ya
maendeleo na shughuli zingine za usimamizi wa maendeleo.
“Njia ya pili ni kupitia mabenki
kwa sababu mabenki yanashirikiana na BoT katika kufanya shughuli zake za
kila siku mabenki hayo yanapohitaji fedha ndiyo Benki Kuu inavyotoa
fedha hizo katika uchumi kwa mabeki.
Katika kipindi cha hivi karibuni
mikopo katika mabenki kwenda kwenye sekta binafsi imeongezeka kwa kiasi
kikubwa kulingana na matarajio na sisi tunaona bado hili liko ndani ya
matarajio yetu”. amesema Dk Misango.
Amesema serikali imekuwa ikifanya
shughuli nyingi za miradi ya maendeleo ambapo inatumia fedha nyingi
ambazo zinaingia kwenye mzunguko.
Hii dhana ya kusema kwenye
mzungukoi hakuna fedha haiko sawa kwa sababu fedha zimekuwa zikiongezeka
katika uchumi kutokana na watu wanaoavyofanya shughuli hizo za
kiuchumi na maendeleo.
Ameongeza kuwa kwa siku za hivi karibuni ongezeko la ujazo wa fedha limekuwa kati ya asilia 8 mpaka 9. Lakini kitu ambacho kimetokea kwenye uchumi ambacho ni muhimu watu wakaelewa ni maendeleo katika mifumo ya malipo.
Mzunguko wa
fedha unaenda kwa haraka zaidi unapata fedha unamlipa mtu A. na Mtu A
naye anamlipa mwingine kwa hiyo mzunguko unakuwa mkubwa kuliko kiwango
kilichokuwa kinatokea zamani, lakini jambo kubwa hapa ni ule mzunguko
wa fedha unatakiwa uuiane na fedha taslimu ambayo inakuwa imetolewa
katika shughuli za uchumi.
Dk. Misango anemalizia na kusema
ingekuwa mzunguko wa fedha umepungua katika uchumi lingekuwa jambo gumu
sana kusema kuhusu ukuaji wa uchumi ambao tumekuwa tukiusema kila
wakati.
No comments :
Post a Comment